Kanye West atunga shairi la kifo siku chache baada ya kuachwa

Muhtasari

• Baada ya kuachana na mkewe Kim Kardashian, Kanye West amewashangaza wengi baada ya kuachia tungo kwa jina 'dead' ambapo anazungumzia kifo.

Kanye West
Image: Instagram

Msanii nguli wa Hiphop Kanye West ametunga shairi la kifo siku chache tu baada ya mahakama moja nchini Marekani kuamua kesi ya talaka ambayo aliyekuwa mkewe wa miaka mingi Kim Kardashian alikuwa amewasilisha.

Kanye West alikuwa kinyume na matakwa hayo ya Kardashian kwani yeye alikuwa analiona suala hilo halikuwa limekaa kisheria zaidi na ni suala la kinyumbani ambalo wangeketi chini na walisuluhishe ili waendelee kulea watoto wao Pamoja lakini Kardashian alipinga vikali na kuelekea Mahakamani ili kumshrutisha mfokaji huyo kumkabidhi talaka yake nqa hivyo kutangazwa rasmi kuwa ‘single’

Tangu kuamuliwa kwa kesi hiyo ambayo West alipoteza, msanii huyo alionekana Dhahiri kudhoofika na msongo wa mawazo na pia kuathirika na unyongovu ambapo alimfurusha wakili wake katika kesi hiyo kwa kushindwa kumtetea ili angalau apate haki ya kusimamisha matakwa ya talaka ya Kim Kardashian.

Siku moja iliyopita West aliandika tungo ya talaka hiyo ambako alikuwa anajieleza jinsi anavyohisi baada ya ya kutenganishwa na ndoa yake ambayo alijitahidi kwa zaidi ya miaka kumi kuistawisha.

Sasa tena ameshangaza wengi Jumanne alipoachia tungo nyingine akizungumzia kifo ambapo mashabiki wake wengi wanahisi msanii huyu amefika mbali kabisa na unyongovu na huenda atachukua maamuzi mabaya sana.

Ninahisi tayari kuathiriwa kwamba ni lazima kuhalalisha usemi wangu baada ya zaidi ya miaka 20 ya sanaa ambayo nimechangia katika sayari lakini pia naona haja ya kuhakikisha sisi kama viumbe tunaruhusiwa kuhisi chochote. Wanaume hawaruhusiwi kulia watu mashuhuri. Siruhusiwi kulia sitakieleza hiki kipande kipya maana maelezo yanaharibu siri na uchawi wa mapenzi ya kweli na kuiweka kwenye box inayoweza kuhesabiwa. Sanaa ni subjective Sanaa inafanya kazi tu wakati ni msanii ukweli mtupu. Ukweli wa mtu unaweza kuwa mwingine. Watu hudanganya. Si lazima sote tuhisi sawa kwa sababu hatufanani. Kwa maelezo zaidi ninawasilisha kwako tungo yangu mpya zaidi inaitwa DEAD.” Aliandika West.

Katika tungo hiyo, Kanye anaelezea kwamba hakuna aliyetaka kuuambia kwamba amekufa na watu tu ambao alikuwa aliwathamini ndio sauti zao zilikuwa zikirindima tu katika kichwa chake.

Hakuna aliyetaka kuniambia kuwa nimekufa. Na ni watu tu ambao wangezungumza nami walikuwa kichwani mwangu,” mwanzo wa tungo hiyo unasema.Jamani mkumbuke kwenye maombi rapa Ye maana huku anakoelekea si kwema kabisa!