Kanye West ampiga kalamu wakili aliyesimamia kesi yake ya Talaka

Muhtasari

•Rapa kutoka Marekani Kanye West amepiga kalamu wakili aliyekuwa akisimamia kesi yake ya talaka na  mkewe Kim Kardarshian.

Image: GETTY IMAGES

Rapa kutoka Marekani Kanye West amepiga kalamu wakili aliyekuwa akisimamia kesi yake ya talaka na  mkewe Kim Kardarshian.

Kanye amekuwa na malumbano ya nyumbani na aliyekuwa mke wake, Kim Kardashian ambaye aliwasilisha ombi la kutaka kutalikiana naye.

Kulingana na mtandao wa TMZ, Kanye  hawajakuwa na uhusiano mwema na wakili  Chris Melcher ikibainika kuwa  mawasiliano yao yamekuwa chache siku za hivi karibuni.

Inasemakana  kuwa kuna wakati Kanye alikuwa anadai kusuluhisha  suala hilo nje ya mahakama.

Rapa huyo  ameajiri wakili Samantha Spector,ambaye hivi majuzi alimwakilisha Nicole Young katika talaka yake na Dk. Dre.

Kesi ya Kanye imeratibiwa  siku ya Jumatatu ijayo, ambapo jaji anatarajiwa kutoa uamuzi wa  talaka yao na Kim rasmi.  

Aidha Kim aliwasisilisha ombi mahakamani la kutaka kutumia video kuwasilisha malalamishi yake na sababu za kuomba talaka.