Kanye West aeleza yaliyomkumba siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanawe

Muhtasari

•Aliyekuwa mpenzi wake wa zamani  Kim Kardarshian alikataa kumwalika kwa sherehe hizo ila rafiki wake wa karibu ndiye alimweleza eneo lililoandaliwa sherehe hizo.  

Mwanamuziki Kanye West
Mwanamuziki Kanye West
Image: Hisani

 Rapa wa Marekani Kanye West alikuwa na furaha kubwa baada ya kuruhisiwa kudhuria sherehe za siku za kuzaliwa za mwanawe Chikago.

Kanye alidai kuwa aliyekuwa mpenzi wake Kim Kardarshian alikataa kumwalika katika sherehe hizo ila rafiki wake wa karibu akamwelekeza hadi  eneo ambapo sherehe ziliandaliwa.

Kulingana na mtandao wa TMZ, mapema siku hiyo Kanye alimshutumu Kim kwa kumzuia kuonana na mtoto wake katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.  

Alisema Kim alikataa kumpa anwani ya sherehe, na kueleza kuwa hio ni mfano wa  jinsi akina baba waliotengwa na familia wanavyopata taabu kuwaona watoto wao.

Kanye alisema alipata habari  kuwa sherehe hio ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Kylie.Pia alishukuru Kris na Corey  kwa kumruhusu kuingia kwenye eneo la Burudani.Alieleza kilicho mshangaza ni kamba walinzi walimuzuia kwa muda mlangoni.