Kanye West alalamika kuhusu wasanii kunyanyaswa na majukwaa ya muziki

Muhtasari

• Rapa na muigizaji wa Marekani Kanye West amelalamika kuhusu  majukwaa ya kueneza muziki yanavyotesa wasanii kwa kuwalipa malipo duni kutokana na kazi zao.

Mwanamuziki Kanye West
Mwanamuziki Kanye West
Image: Hisani

Rapa na muigizaji wa Marekani Kanye West amelalamika kuhusu  majukwaa ya kusambaza muziki yanavyotesa wasanii kwa kuwalipa malipo duni kutokana na kazi zao.

Kulingana naye, majukwaa ya muziki yamekuwa yakiwadhulumu wasanii kwa muda mrefu kwa kuwalipa pesa kidogo  kutokana na kazi zao za sanaa.

Baadhi ya majukwaa ya kusambaza muziki ni YouTube, Apple, Amazon na Spotify.

Vilevile, alisema wasanii hulipwa  asilimia 12 kutokana na kazi zao huku majukwaa hayo yakipokea asilimia kubwa

"Kwa sasa wasanii wanapata asilimia 12 tu, kutokana na kazi zao,  wakati umefika kuachana na mfumo huu unaowanyanyasa wasanii, ni wakati wa kuchukua udhibiti na kujenga  majukwaa yetu wenyewe,”alisema Kanye West.

Ni majuzi tu msanii wa humu nchini Vivianne alilalamikia kampuni moja ya kusambaza muziki kwa malipo duni kutokana na kazi zao.

Kanye West ameeleza mashabiki wake kuwa amefungua App mpya ambayo atakuwa anapakia muziki wake na kusambaza yeye mwenyewe bila usaidizi wa majukwaa mengine.