Ninatazamia kuongeza watoto 4 zaidi - Akothee

Muhtasari

• Akothee ametangaza kuwa mipango yake kabla ya kufika miaka 45 ni kuongeza watoto wanne zaidi

• Pia ametangaza atastaafu kutoka maisha ya uwazi na kukumbatia maisha ya faragha atakapofika miaka 45

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki mashuhuri wa kike nchini Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amewaacha wengi vinywa wazi baada ya kuzungumzia Maisha yake miaka minane iliyopita na pia kuzungumzia maazimio yake ya miaka minane ijayo

Mama huyo wa watoto watano alisema katika miaka minane ijayo, anatazamia kuongeza watoto wanne Zaidi kabla ya kustaafu kutoka Maisha ya uwazi akiwa na miaka 45.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Akothee alisema kwamba miaka minane iliyopita alikuwa tayari ashanunua shamba kijijini mwao n ahata kujenga nyumba

Akothee alifichua kwamba katika muda wa miaka miwili ijayo, atakuwa anatimiza mwongo mmoja wa kujitunza vyema na kubaia vilr vile alivyokuwa miaka minane iliyopita.

Msanii huyo mwenye vitimbi kila mara alisema kwamba atakapostaafu kutoka muziki atarudi kijijini kwa nyumba yake aliyoijenga miaka minane iliyopita na kudokeza kwamba ataanza Maisha mapya ambayo si ya kujitangaza mitandaoni na kuzaa watoto wanne Zaidi

“Miaka minane ijayo, nitakuwa nastaafu kwa miaka 45, nitakuwa naanzisha familia mpya ya Maisha ya faragha na ninatarajia kuongeza watoto wanne Zaidi, nitakuwa katika nyumba yangu ya kustaafu na pia nitatoka kabisa katika Maisha ya umaarufu na kukumbatia Maisha ya faragha,” aliandika Akothee