Nimeblock akaunti 500 tangu 2022 - Akothee

Muhtasari

• Mwanamuziki na mfanyibiashara Esther Akoth almaarufu Akothee amesema tangu mwaka wa 2022 kuanza, tayari ameblock akaunti zaidi ya mia tano mitandaoni.

• Amesema aliamua kuanza kuchukua hatua hiyo kwa sababu hana muda tena wa kujibizana ovyo mitandaoni.

Akothee
Image: Facebook

Mwanamuziki na mfanyibiashara Esther Akoth almaarufu Akothee amesema tangu mwaka wa 2022 kuanza, tayari ameblock akaunti zaidi ya mia tano mitandaoni.

Akothee anasema hatua yake hiyo ya kublock akaunts za watu ambao wana mazoea ya kutukana na kusimanga mitandaoni.

Amesema aliamua kuanza kuchukua hatua hiyo kwa sababu hana muda tena wa kujibizana ovyo mitandaoni.

Image: Instagram

“Ooh kwa taarifa yenu tayari nimeblock akaunti 500 tangu 2022 inanze. Hii ndio njia mbadala ya kuwalinda kwa sababu hamuwezi futa ufuasi. Sina tena muda wa kubishana, kwa sababu huenda umelipwa kubishana na mimi. Nahitaji muda wa kufanya vitu vya maana. Huu ukurasa ni wangu,” aliandika Akothee

Akothee ambaye amekuwa akisimangwa mitandaoni anaonekana kuwa kama baharia kwani kusimangwa sasa kumekuwa mazoea kwake na haonekani kutishika na suala hilo.

Itakumbukwa msanii huyo aliwahi geuzwa kiungo cha mjadala mitandaoni wakati wakenya walikuwa wanajaribu kumfananisha na msanii Beyonce

“Kama kusimangwa mitandao kungekuwa ni jeneza basi wakenya wangeuzwa majeneza mengi sana nje ya nchi. Wanataka Beyonce lakini Akothee ndio yuko,” aliandika Akothee

Msanii huyo amekuwa akigonga vichwa vya habari katika wiki za hivi karibuni baada ya mfanyakazi wake wa zamani kumsema kwamba alikuwa ameshikilia mshahara wake kwa muda mrefu.