Umaskini unaleta unyama kwa watu-Akothee

Muhtasari
  • Akothee alivuma wiki jana kwa madai tofauti huku akichukua fursa hiyo na kuzungumzia madai hayo
  • Pia ni mmoja wa wasanii ambao wamefahamika sana kupitia bidii ya kazi yao katika tasnia ya muziki
MADAM BOSS
MADAM BOSS

Msanii maarufu Esther Akoth,almaarufu Akothee amekuwa akiwashawishi mashabiki wake kwa njia moja au nyingine, huku neno lake kuu ni kutia bidii katika kila jambo.

Akothee alivuma wiki jana kwa madai tofauti huku akichukua fursa hiyo na kuzungumzia madai hayo.

Pia ni mmoja wa wasanii ambao wamefahamika sana kupitia bidii ya kazi yao katika tasnia ya muziki.

Mama huyo watoto 5 na mjasirimali hajakuwa akifuata yale wakaosaji wake wamekuwa wakisema bali amekuwa akikabiliana nao vipasavyo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amezungumzia jinsi umaskini unaweza kuleta unyama kati ya binadamu.

Pia amesema kuwa watu wengi wakpata pesa na umaarufu hubadilika.

"Umaskini unaleta unyama kwa watu! Utajiri huleta wewe halisi! Watu wengi si wanyenyekevu, hawana pesa! Subiri hadi wapate pesa kidogo na umaarufu! Utawajua 💪."