“Nilivunjika kabla nijengwe” Akothee afunguka kuhusu harusi yake rahisi iliyogharimu 2000

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto watano amefichua kwamba harusi hiyo haikuwa kubwa na iliwagharimu shilingi elfu mbili tu.

•Akothee amewashauri watu kutopoteza matumaini ya maisha na kuendelea kupambana huku akijitumia kama mfano bora wa matunda ya uvumilivu.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almarufu kama Akothee amefichua  kwamba alifanya harusi rahisi na baba wa binti zake watatu, Jared Okello.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Akothee ameeleza kwamba mpenzi wake wa zamani alisisitiza wafunge pingu za maisha wakati alikuwa anapanga kusafiri nje ya nchi kwa kuwa alihitaji kuenda na hati ya harusi. 

Mama huyo wa watoto watano amefichua kwamba harusi hiyo haikuwa kubwa na iliwagharimu shilingi elfu mbili tu. Alisema kulikuwa na gari moja tu katika harusi yake ambalo waliomba kutoka kwa rafiki yao.

"Katika siku yangu kubwa ya harusi! Ilitubidi kufanya  harusi hii kwa kuwa mume wangu alikuwa asafiri kwenda Bahamas! Alitaka kwenda na cheti cha ndoa yetu ili iwe rahisi kwake kutualika., Nilikuwa natazamia kuingia Amerika hivi. Harusi yangu iligharimu 2000sh. Tuliomba gari moja tu kutoka kwa rafiki" Akothee alisema.

Mwanamuziki huyo amesema kwamba siku hiyo ya harusi alipatwa na huzuni ila hakufahamu sababu zilizochangia hali ile.

Akothee amewashauri watu kutopoteza matumaini ya maisha na kuendelea kupambana huku akijitumia kama mfano bora wa matunda ya uvumilivu.

"Usiwahi kukufa moyo! Usiwahi kuacha! Endelea kusukuma! Nilikuwa mdhaifu kabla ya kufanikiwa... Wewe sio mwenye sura baya, wewe sio mnyonge! Wewe huna pesa lakini hujavunjika" Akothee alisema.

Akothee na bw Okello walitengana miaka mingi iliyopita wakati kifungua mimba wao Vesha Okello alikuwa katika darasa la nne.