Magonjwa yaliyokuwa yameshambulia mchekeshaji Akuku Danger hadi kulazwa hospitalini tena yafichuliwa

Muhtasari

•Silprosa alitangaza kuwa madaktari tayari wamemruhusu kutoka hospitalini baada ya kubaini kuwa afya yake ni imara.

•Mwigizaji huyo wa Auntie Boss vilevile alifichua kuwa Akuku alilazwa hospitalini baada ya kupatikana na ugonjwa wa moyo, pneumonia na kifua kikuu.

Magonjwa yaliyokuwa yameshambulia Akuku Danger yafichuliwa
Magonjwa yaliyokuwa yameshambulia Akuku Danger yafichuliwa
Image: INSTAGRAM// SANDRA DACHA

Mchekeshaji wa Churchill Show Akuku Danger amefanikiwa kupata afueni baada ya kulazwa hospitalini kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Siku ya Jumatatu, mwandani wa  Akuku Danger, Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa alitangaza kuwa madaktari tayari wamemruhusu kutoka hospitalini baada ya kubaini kuwa afya yake ni imara.

Dacha alisema kuwa Akuku Danger angeendelea kupumzika na kukunywa dawa zake baada ya kufika nyumbani.

"Tunafurahi kwamba Akuku kwa mara nyingine tena anaruhusiwa kutoka Hospitalini ya Nairobi West. Sasa anaweza kwenda nyumbani na atakuwa anapumzika kitandani kwani bado anatumia dawa. Tunatoa shukrani.  Asanteni sana kwa kusimama na Akuku Danger katika safari hii yote" Dacha aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Dacha aliambatanisha ujumbe wake na video iliyoonyesha akisherehekea pamoja na mchekeshaji huyo ambaye hivi majuzi alitambulisha kama mpenzi wake.

Mwigizaji huyo wa Auntie Boss vilevile alifichua kuwa Akuku alilazwa hospitalini baada ya kupatikana na ugonjwa wa moyo, pneumonia na kifua kikuu.

“Baada ya kulazwa hospitalini tena wiki iliyopita kufuatia kupatikana na maambukizi mapya ya moyo, pneumonia na kifua kikuu, tuko na raha kuwa Akuku anaruhusiwa tena kuenda nyumbani kutoka hospitali ya Nairobi” Dacha alisema.

Hata hivyo aliendelea kutoa wito kwa Wakenya kusaidia katika kuchanga bili ya hospitali ambayo imeendelea kupanda.