Ogopa Mungu na umaskini pekee -Akothee

Muhtasari
  • Aidha msanii huyo aiwashauri mashabiki wake wasali kwenye ndoa zao, kwani ndoa ni kitu muhimu
Image: INSTAGRAM

Msanii na mjasirimali maarufu Esther Akoth almaarufu kama Akothee kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amepakia picha yake ya zamani huku akiwahimiza mashabiki wake waogope Mungu.

Zaidi ya yote aliwashauri mashabiki wake waogope umaskini, Akothee anafahamika sana kwa bidii ya kazi yake.

Aidha msanii huyo aiwashauri mashabiki wake wasali kwenye ndoa zao, kwani ndoa ni kitu muhimu.

"Happy Sabbath! From My SDA family! 🤣🤣🤣Uwiiiii Ogopa Mungu na umaskini pekee 🤣🤣🤣Wengine wote ni Bure kabisa🤣🤣👋Marriage is sweet guys ,stay in your marriage," Aliandika Akothee.

Wiki hii msanii huyo amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya aliyekuwa mfanyakazi yake kuai kwamba amekataa kumlipa mshahara wa miezi 2.

Akothe alijitokeza na kuzungumzia madai hayo, na kueleza haswa nini kilitendeka kati ake na mfanyakazi huyo.