Kauli ya Diamond platnumz kwa wapenzi wa Kiswahili

Muhtasari

•Lugha ya kiswahili imekuwa miongoni mwa lugha ishirini ambazo zinazozungumzwa sana dunia.

•Amesifia lugha ya kiswahili na kueleza kuwa   faraja yake nikuona  lugha ya kiswahili imeenea na kukua na kufikia  kiwango cha Kimataifa ambacho kila anayezungumza lugha hiyo atakuwa anajivunia

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: Hisani

Mwanamuziki nguli Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platnumz  amesifia lugha ya Kiswahili na kueleza kuwa faraja yake nikuona  lugha ya Kiswahili imeenea na kufikia  kiwango cha Kimataifa ambacho kila anayezungumza lugha hiyo atakuwa anajivunia.

Lugha ya Kiswahili imekuwa miongoni mwa lugha ishirini ambazo zinazungumzwa sana dunian.

Kupitia ukurusu wake wa Instastori ameeleza nia yake kila wakati ni kufanya wazungumzaji wa lugha ya kiswahili kujisikia  na kujivunia lugha wanapozungumza  furaha wakati wanazungumza  Duniani.

"Faraja yangu ni kufanya kila anaeongeoa Kiswahili kutembea kifua mbele popote duniani,” alisema Diamond Platnumz.

Kauli hii imewadia baada ya msanii Rayvanny kufanya show ya kibabe nchini  Dubai ambapo mashabiki  walifurika na kujaza ukumbi.

Vilevile aliwaomba wasanii ambao wanaimba kutumia lugha ya Kiswahili kushirikiana ili kueneza lugha ya Kiswahili kuendelea kuwa kipenzi cha wengi duniani.

Kwa mashabiki aliwaomba waache tabia ya kutoshanisha wasanii wanaotumia lugha hiyo na kuanza kuweka mizani moja na wale wanatumia lugha zingine.