Sipo tayari kupenda tena! - Carrol Sonie afunguka

Muhtasari

• Aliyekuwa mke wa mchekeshaji Mulamwah, Carrol Sonie amefunguka na kusema kwamba mapenzi yalimtenda vibaya sana na katu hayuko tayari kuingia katika mahusiano tena.

• Ila alisemqa kwamba anaamini mapenzi ya kweli yapo na kama yatakuja upande wake siku za mbeleni basi atayakubali na kuyapokea.

Carrol Sonie
Image: Facebook

Aliyekuwa mke wa mchekeshaji Mulamwah, Carrol Sonie amefunguka na kusema kwamba mapenzi yalimtenda vibaya sana na katu hayuko tayari kuingia katika mahusiano tena.

Sonie ambaye ni muigizaji waliachana na Mulamwah mwishoni mwa mwaka jana katika kile ambacho wengi hawakuamini kwa kudhania wawili hao walikuwa wanafukuzia kiki mitandaoni.

Akizungumza na mashabiki wake kwenye Q&A aliyoifanya kwenye mtandao wake wa YouTube, Sonie alisema kwamba mapenzi yalimshinda na hadhani kama atawahi penda tena ila akasisitiza kwamba anaamini mapenzi ya kweli yapo.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba hata ingawa kwa sasa hana mipango tena ya kupenda wala kuingia katika mahusiano, bado Imani zake zinamtuma kusema kwamba mapenzi ya kweli yapo na kama siku moja yatabisha hodi nafsini mwake basi atayakaribisha na kuyadakia mithili ya tumbili adakiavyo ndizi.

"Mapenzi imepiga Ile kitu. I am not planning to fall in love again but if it happens to come my way, I will not hesitate, I believe love exists," alisema Sonie

Wawili hao waliachana mwishoni mwa mwaka jana na hakuna mmoja kati yao alijitolea kusema ukweli wa kile kilichowatenganisha na katika Q&A hiyo, Sonie alipoulizwa kuhusu suala hilo, alichorea nje na akasema kwamba kama wameachana na mtu hakuna haja ya kushinda kuzungumzia hilo.

“Mtu anataka nimpe ushauri kwa sababu mimi singependa kuzungumzia kuhusu mapenzi yangu ama mahusiano yangu ya awali. Kama mumeachana na mtu, muacha bana, acha kushinda mkiongelelea stori zake. Tusizungumzie hilo,” alisema Sonie.