Diamond Platnumz tayari kuachia album mwaka huu?

Muhtasari

• Msanii kutoka Tanzania, Diamond Platinumz amedokeza kwamba huenda sasa mashabiki wake wakaanza kupokea kazi ambazo wamekuwa wakisubiri sana kutoka kwake.

• Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa instagra, Simba amesema kwamba sasa yupo tayari kutoa miziki yake mipya mwaka huu nwa 2022.

Diamondplatnumz
Diamondplatnumz
Image: Instagram KWA HISANI

Msanii kutoka Tanzania, Diamond Platinumz amedokeza kwamba huenda sasa mashabiki wake wakaanza kupokea kazi ambazo wamekuwa wakisubiri sana kutoka kwake.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa instagra, Simba amesema kwamba sasa yupo tayari kutoa miziki yake mipya mwaka huu nwa 2022.

“Niko tayari 2022,”aliandika Diamond Platinumz.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana Diamond Platinumz alitangaza mara kadhaa kwamba album yake ishakamilika na pia tulishuhudia mara kadhaa akiwa anasafir kwenda nji za nje kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya kazi hizo ambazo hakuwahi kusema tarehe rasmi ya kuziachilia.

Aidha, Platinumz kupitia instagram stories ameachia ujumbe akisema kwamba ushindani ni mzuri ila sasa imefikia kipindi ambapo watanzania wanapswa kuwalinganisha wasanii wao na wale wa kimataifa ili kuhakikisha kwamba muzikiwao unafika katika viwango vya nkimataifa.

Ameongezea kwamba kuwapiganisha wasanii wa bongo haijengi gemu la burudani ila inachangia pakubwa kutojenga mazingira kutoa kazi ambazo zinaweza mkuleta ushindani katika majukwaa ya kitaifa.

Kwa sasa mashabki wanasubiri kwa hamu na ghamu kusikiliza na kutazama kazi kutoka kwa gwiji huo pindi zitakapokuwa tayari.