Jay-Z, Kanye West waongoza chati za marapper bora wa 2021

Muhtasari

• Jay-Z na Kanye West waongoza orodha ya wasanii wa Hip hop walivuna pakubwa kifedha katika mwaka wa 2021 kwa jumla ya $720M.

Jay-Z, Kanye West
Image: Instagram

Aliyekuwa mhariri wa Forbes Zack O’Malley Greenburg ametoa orodha ya wasanii nguli wa mtindo wa kufokafoka wa rap na hip-hop ambao walifana sana katika mwaka wa 2021. Greenburg amekuwa akifanya utafiti na kuunda orodha ya wasanii wa rap na mambo mengine mbalimbali yanayohusiana na mtindo huo wa muziki kwa Zaidi ya miaka kumi akiwa na Forbes.

Orodha hiyo inaonesha wasanii wa hip-hop ambao walilipwa Zaidi kwa mwaka huo kutokana na kazi zao kuchezwa na kupakuliwa kutoka majukwaa mbalimbali ya kusambaza miziki Pamoja na matamasha ambayo walitumbuiza.

Orodha hiyo imetawaliwa na wasanii nguli kutokan Marekani ambako ndilo taifa linajulikana sana kwa miziki ya rap na hiphop.

Jay-Z ameongoza kwa kuwa msanii aliyevuna pakubwa mwaka wa 2021 kutoka kwa kazi zake ya Muziki ambako alijizolea takribani $470M, kiwango ambacho kinatajwa kuwa kikubwqa Zaidi kwa msanii huyo kuwahi kupokea kwa mwaka kutokana na kazi zake za muziki.

Huyu ni kama hakuathirika na janga la Corona ambalo limevuruga shughuli nyingi tu kote ulimwenguni.

Akifuatiwa kwa umbali ni msanii Kanye West ambaye licha ya ndoa yake na mwanamitindo Kim Kardashian kuwa na misukosuko mingi katika mwaka wa 2021 na baadae kuvunjika, alijitahidi sana kimuziki na kutia kibindoni $250M huku akifunga tatu bora ni msanii Diddy ambaye alipata $75M kwa mwaka huo. Kwa jumla, mapato ya watatu hao yanagonga $800M, kiwango ambacho ni kikubwa Zaidi kuwahi kutokea kwa wasanii hao na kiwango hiki kinatajwa kuwa karibia mara mbili Zaidi ya kabla ya janga la Corona.

Ni kama watu wengi walianza kununua na kusikiliza miziki hii wakati janga hilo lilipobisha na wengi kulazimika kusalia majumbani ili kukwepa maambukizi.

Pia jambo lingine la kuwatia moyo watoto wa kike ni kwamba katika orodha hiyo, msanii wa kike Doja Cat alishikilia nafasi ya kumi Pamoja na wasanii Birdman na Tech N9ne ambao wote walikuwa na mapato ya $25 kila mmoja katika kufunga kumi bora.

Hii ni taarifa njema kwa usawasishaji wa kijinsia kwani muziki wa hip hop kwa muda mrefu umekuwa ukihusishwa pakubwa na watoto wa kiume lakini sasa Doja Cat anawapa motisha watoto wa kike ambao wana talanta katika kuimba miziki na aina hiyo kwamba nafasi ipo na wataweza.

HipHop DX
Image: Twitter