Babalevo asema mwaka huu Diamond atawazima wasanii wengi

Muhtasari

• Msanii kutoka Tanzania, Babalevo amesema kwamba mwaka huu Diamond Platinumz anakwenda kufanya mambo mengi makubwa na kuwatoa kijasho wasanii wenzake katika gemu la burudani.

• “Diamond alisema mwaka huu anakwenda kufanana na hela zake, watu watachoka sana na kazi,” Babalevo alisema.

Msanii kutoka Tanzania, Babalevo amesema kwamba mwaka huu Diamond Platinumz anakwenda kufanya mambo mengi makubwa na kuwatoa kijasho wasanii wenzake katika gemu la burudani.

 Akizungumza Alhamisi katika uzinduzi wa EP ya Diamond Platinumz, Babalevo alisema kwamba kutokana na wingi wa hela alizonazo Simba, atakuwa anaachia kazi kali ambazo zitabaki kwenye kumbukumbu.

“Diamond alisema mwaka huu anakwenda kufanana na hela zake, watu watachoka sana na kazi,” Babalevo alisema.

Babalevo alisisitiza kwamba Simba ndiye msanii wa kipekee ambaye anaweza kupeleka muziki wa bongo katika viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake alisema muda rasmi hujawadia kwake kuachia EP akisema anataka kupata mashabiki wa kutosha.

Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mtangazaji katika Wasafi fm, ni moja kati ya watu ambao ni ‘chawa’ wake Diamond Platinumz.

Kwa sasa inasubiriwa kuona EP hiyo itafanya vipi katika gemu la Bongo na Afrika Mashariki.