Ulishindwa kusimamia wasanii, siasa utaweza? mashabiki wamchamba Bahati

Muhtasari

• Mashabiki wamemjia juu msanii Bahati baada ya kuchapisha ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram ambapo alijitambua kama mbunge mtarajiwa wa eneo la Mathare.

• "If managing a few artist ilikushinda, constituency ndo utaweza?" achitsal aliandika.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Bahati kenya

Mashabiki wamemjia juu msanii Bahati baada ya kuchapisha ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram ambapo alijitambua kama mbunge mtarajiwa wa eneo la Mathare.

"Habari za asubuhi kutoka kwa mbunge mtarajiwa wa eneo la Mathare, niambie unawakilisha eneo lipi," Bahati aliandika.

Kuna baadhi ya mashabiki ambao walionekana kutomuunga mkono katika azma hiyo ya uongozi wakimtaka azidi kujishughulisha na kazi zake za muziki.

"Broh ni jokes utaacha tulia studio bana 😂😂," edwin_lewis_jnr aliandika.

Aidha, kuna wale waliomtupia cheche kali kwa kukosa kufanikiwa kuwasimamia wasanii waliokuwa chini ya lebo yake, wakishangaa angewezaje kuongoza eneobunge hilo na kuleta maendeleo kwa wakazi.

"If managing a few artist ilikushinda, constituency ndo utaweza?" achitsal aliandika.

Asilimia fulani ya mashabiki pia walionekana kuiunga azma yake mkono wakimpa  hakikisho kwamba lazima atashinda.

"Good morning our incoming muheshimiwa watu wa mathare zoea mp wako mapema," shabiki mwengine alisema.

Bahati anaongezea orodha ya wasanii ambao wamejitosa katika kivumbi cha Agosti 9, huku wakitoa ahadi ya kubadilisha maisha ya vijana.