WCB inakupa likes, Zuchu amlipua mwanahabari wa Clouds Fm

Muhtasari

• Msanii Zuchu ameamua kumtupia maneno makali mtangazaji wa Clouds fm aliyejaribu kukosoa video ya ngoma #Mtasubiri.

• Amemwambia kwamba vurugu hizo haziwezi kumfaidi lolote, ila likes a views chache tu.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Zuchu

Mwanamuziki wa WCB, Zuchu amemtupia maneno makali mtangazaji wa Clouds fm Soudybrown baada ya mtangazaji huyo kuonekana kuikosoa video ya wimbo #Mtasubiri ambapo Zuchu alishirikishwa na Diamond Platnumz.

Kipande cha kwanza cha video hiyo ambacho Soudybrown alikikosoa, ni pale ambapo Zuchu anaondoka kanisani ili kukutana na mpenzi wake ambaye kulingana na video hiyo ni Diamond.

"Umefanya vizuri kwenye hii video, ila ndo kutoroka kanisani kufuata mapenzi? Una balaa wewe," alisema.

Sehemu ya pili ambayo pia mtagazaji huyo alioekana kuwa na tatizo nayo ni pale ambapo Zuchu amepanda bodaboda bila kuvalia kofia ya kujikinga [helmet]wakati unapotumia usafiri huo.

"...Nikuambie ukweli, anayekupenda hawezi kuruhusu uwe kwenye hatari kubwa kama hii," Soudy aliandika.

Kwa upande wake Zuchu alionekana kutofurahishwa na kitendo hicho na kuamua kumjibu kwenye 'comment section.'

"Naelewa mwaya unatafuta zako riziki hali ni ngumu upande wenu walau vitu kama hivi vinakupa likes na comments ," Zuchu aliandika.

Ghadhabu ya Zuchu imetokana na hali kwamba Soudybrown hajakuwa akiangazia mambo ya wasanii wa Wasafi kwa kuwa ameegemea sana upande wa Alikiba na Harmonize, ila ghafla tu akaanza kukosoa kazi zao.

Kulingana na Zuchu, mtangazaji huyo anaweza tu kupata umaarufu  anapowazungumzia wasanii wa lebo ya Wasafi.