Hisia kemkem baada ya Massawe Japanni kuwa mfawidhi kwenye sikukuu ya Madaraka

Muhtasari
  • Katika hafla hiyo, watangazaji hao wawili walipata fursa ya kucheza majukumu yao ambayo kwa kawaida huigiza wakiwa studio
MTANGAZAJI MASSAWE JAPANNI
Image: RADIOJAMBO/FACEBOOK

Huku Wakenya wakisherehekea sikukuu ya Madaraka, Rais Uhuru Kenytta aliliongoza taifa katika bustani ya Uhuru ili kusherehekea sikukuu hiyo.

Ilikuwa sikukuu ya 59 tangu Kenya kupata Uhuru, wanasiasa,wananchi na wageni waalikwa walihudhuria sherehe hizo.

Katika upande wa burudani, mashabiki hawakulaza damu na tabasamu zao baada ya kumuona mtangazaji wa Radiojambo Massawe Japanni na Mzazi Tuva wakiwa wafawidhi wa siku.

Katika hafla hiyo, watangazaji hao wawili walipata fursa ya kucheza majukumu yao ambayo kwa kawaida huigiza wakiwa studio.

Willy M Tuva wa Radio Citizen na Massawe Japanni wa Radio Jambo walipewa jukumu la kuwa wafawidhi katika hafla hiyo.

Waliwakaribisha wachezaji mbalimbali uwanjani, wakianza na watoto wanaoanzisha mfumo mpya wa elimu, Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC) kwa wasanii wa kitamaduni kutoka kote nchini ambao walipewa nafasi ya kutumbuiza.

Rais Uhuru Kenyatta aliburudishwa na wasanii hao huku akionekana akitabasamu kwa mbali na baadhi ya nyakati akipiga makofi.

Madaraka 59 ilikuwa tofauti ya aina yake na tamaduni mbalimbali zilizopewa nafasi ya kuonyesha mazoezi yao kupitia nyimbo na ngoma.

Mashabiki walitoa hisia zao tofauti kwa wawili hao kuwa wafawidhi katika sherehe hizo.