Muigizaji mkongwe wa filamu aonekana mitaani akiwa maskini wa kuombaomba

Mugizaji Kenneth Aguba alifana sana kipindi cha nyota yake ikiwa angavu ambapo alicheza filamu kadha maarufu.

Muhtasari

• Mhubiri mmoja kwa jina Chibuzor Chinyere alijitolea na kumpa makaazi kabla ya kumpeleka hospitali.

• Muigizaji huyo picha zake zilivujishwa akiomba omba mitaani kama chokoraa.

Muigizaji mkongwe wa Nigeria Kenneth Aguba akiwa katika umaskini wa kuomba omba mitaani
Muigizaji mkongwe wa Nigeria Kenneth Aguba akiwa katika umaskini wa kuomba omba mitaani
Image: TWITTER

Muigizaji mkongwe kutokea nchini Nigeria kwa jina Kenneth Aguba ambaye juzi aliripotiwa kuzama katika umaskini mkubwa hadi kugeuka omba omba mitaani asiyekuwa na makao, hatimaye amezawadiwa nyumba.

Muigizaji huyo mkongwe juzi kati picha zake akiwa omba omba mitaani huku hali yake ikiwa ya kutia huruma licha ya kuwa maarufu aliyecheza katika filamu mbali mbali zilizofanya vizuri, hali yake iliwavunja wengi wa mashabiki wake.

Picha hizo zilivujishwa mitandaoni ambapo zimekuwa zikisambazwa pakubwa baadhi wakiilaumu uongozi wa wasanii wa filamu nchini humo kwa kumtelekeza na kupelekea yeye kurambwa na umaskini hadi kukosa makao maalumu.

Baada ya picha hizo za kutia huruma kusambaa, mhubiri mmoja mwanzilishi wa kanisa la Omega Power Ministry kwa jina Chibuzor Chinyere amemzawidi nyumba ya kifahari katika mji wa Port Harcourt nchini Nigeria.

Inaarifiwa kwamba pia mchungaji huyo alimpeleka muigizaji Aguba katika hospitali ya kupima watu akili ili akafanyiwe ukaguzi wa kiakili na kupata matibabu iwapo ameathirika.

Kando na kumpa makazi, mchungaji huyo pia alitangaza kumtafutia Aguba mke, jambo ambalo limeibua wanawake wengi wa kila aina kila mmoja akitaka kuchukuliwa kama mke wa muigizaji Aguba, haswa baada ya kuona nyota yake ikitiwa mwanga tena ila kipindi yupo omba omba mitaani kila mwanadada alikuwa anamnyea na kumuona kama kinyesi cha sokwe ashakum si matusi.

Wapenzi wa filamu za Nigeria wanamkumbuka Kenneth Aguba ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 71, katika filamu mbali mbali alizocheza enzi nyota yake inang’aa.

Baadhi ya filamu ambazo nyota huyo wa kuigiza alicheza ni pamoja na ile ya Fire on the Throne, Secret Palace, Blood Rain, Perfect Kingdom miongoni mwa filamu moto zilizotikiza katika nchi nyingi na kuipa Nigeria sura ya uigizaji barani Afrika.