(Video) "Natafuta mtu wa kunichekesha kwa malipo, atakaa na mimi saa 24" - Irene Uwoya

Alisema anataka mtu wa kumchekesha kwa sababu kichwa kinauma kutokana na mambo mengi ya kutafuta maisha.

Muhtasari

• "Kama ni wewe ama kuna mtu unayemjua anajua kuchekesha yaani kazi ni kunichekesha tu nitamlipa vizuri." - Uwoya

Muigizaji na mfanyibiashara Irene Uwoya ameweka wazi kwqamba anatafuta mtu wa kumpa kazi ya kumchekesha tu saa ishirini na nne kwa siku.

Mwanamama huyo aliweka wazi kwamba mtu huyo lazima ajue kuchekesha na atakuwa anaandamana naye kila siku na kukaa naye saa zote ishirini na nne huku kazi yake kubwa na ya kipekee ikiwa ni kumvunja mbavu tu na kujiingizia posho nono mfukoni kila baada ya mwisho wa mwezi.

Uwoya alipakia video fupi kwenye ukurasa wake wa Instagram akitaka watu wamsaidie kumuunganisha na mtu ambaye ana uwezo wa kumchekesha ili apate kumpa kazi kwa sababu ana majukumu mengi sana ambayo yamuuma kichwa na anataka kupata Faraja kwa kicheko.

“Hello wadau, sasa nilikuwa na kitu naomba mnisaidie, kutokana na majukumu mengi mambo yanakuwa mengi sana mpaka kichwa kinauma kwa ajili ya kutafuta maisha, nahitaji mtu wa kunichekesha kiukweli, mtu ambaye atakuwa anatembea na mimi saa 24 kwa ajili ya kunichekesha tu, hana kazi nyingine zaidi ya kunichekesha. Mimi nitamlipa, kwa hiyo kama ni wewe ama kuna mtu unayemjua anajua kuchekesha yaani kazi ni kunichekesha tu nitamlipa vizuri. Nitashukuru sana kaam mtanisaidia na hilo,” Irene Uwoya alisema.

Muigizaji huyo mkongwe wiki jana aligonga vichwa vya habari baada ya mchungaji mmoja nchini humo kuweka wazi kwamba yeye ndiye aliyekuwa mgeni wa heshima katika ibada kuu ya kanisa hilo lililokuwa likisherehekea miaka 10 tangu kuanzisha kutoa huduma kwa waumini.

Baadhi walidai ameokoka huku wengine wakisema ni biashara tu kama biashara zingine ambazo mtu anaweza akaitwa kuwakilisha kwenye kumbi za starehe, kama bado hilo halijaisha, tena amekuja na jipya anataka mchekeshaji wa kuwa karibu naye.

Ina maana Afrika Mashariki hamna mtu anayejiamini kabisa kwa kipaji cha kuchekesha? Maana hii ni siku ya pili na bado mchekeshaji hajapatikana na Uwoya anazidi kusaka mtu wa kumchekesha kwa malipo. Kazi kwenu wacheshi!