Wema Sepetu afunguka kuhusu ugomvi wake na Amber Lulu

Muhtasari

•Wema alidhirisha kuwa kwa sasa uhusiano wake na Lulu ni mzuri huku akiwasihi watu wengine kutoingilia uhusiano wao.

Wema Sepetu na Amber Lulu
Wema Sepetu na Amber Lulu
Image: INSTAGRAM

Mwigizaji Wema Sepetu ameweka wazi kuwa hakuna ugomvi wowote kati yake na mwanasoshalaiti Amber Lulu.

Siku chache zilizopatana kulichimbuka wasiwasi kuhusiana na uhusiano wa wasanii hao baada yao kuonekana wakivurutana siku kadhaa zilizopita.

Akizungumzia hayo, Wema amesema drama zilitokea baada  yake na 'Drama Queens' wenzake kukosa kutofautiana kuhusu masuala yao ya ndani.

"Ilikuwa tu ni kutoelewana  baina yangu na wenzangu. Lakini mliona tulikaa sawa. Tumeshapatana. Maisha yanaendelea na mipango ya kazi ipo mingi," Wema alisema katika mahojiano na wanahabari.

Wema alidhirisha kuwa kwa sasa uhusiano wake na Lulu ni mzuri huku akiwasihi watu wengine kutoingilia uhusiano wao.

"Tuko vizuri kabisa. Alafu Lulu ni mdogo wangu. Yule nikiamua namshika nampiga vibaya namwambia tulia. Nyinyi mkiona tukigombana msishadidie. Watu washike jembe wakalime. Kugombana ni vitu vya kawaida. Tunaweza tukagombana mkaingilia mkaja kuona aibu nyinyi mwishowe," Alisema.

Mwigizaji huyo alitangaza kuwa kuna shoo inayoandaliwa ambayo itamhusisha yeye pamoja na Irene Uwoya, Amber Lulu, Kajala Masanja, Auntie Ezekiel na Jacquline Wolper.

Sita hao wamejibandika majina 'Drama Queens' na 'Big Six'. Wamewasihi mashabiki kuwapokea ni kuunga mkono kazi zao.