"Nani anaweza fanya Bora kuliko Binti yangu" Harmonize asifia densi ya Paula

Harmonize anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake Fridah Kajala, mamake Paula.

Muhtasari

• Itakumbukwa juzi pia Paula alimkubali Harmonize na kwa mara ya kwanza kumuita baba licha ya awali kukataa kumtambua baada ya kumvisha mamake pete ya uchumba.

Bintiye Kajala Masanja na babake wa kambo, Harmonize
Bintiye Kajala Masanja na babake wa kambo, Harmonize
Image: Instagram

Harmonize ni baba wa kambo mwenye furaha na Faraja kubwa kwa mwanawe, binti Paula Kajala, ambaye kwa hesabu ya haraka tu ni kama ameachana na babake wa kambo kwa miaka chini ya kumi.

Juzi binti huyo aliwasifia sana Harmonize na mamake Kajala Masanja baada ya wachumba hao kupakia klipu kwenye Instagram wakicheza ngoma zao mpya za Amelowa na Nitaubeba.

Katika ujumbe huo, ambao ni kwa mara ya kwanza alionekana akimkubali Harmonize kama baba yake, Paula aliwasifia kwa kusema kwamba wanajua kudensi mpaka basi.

Itakumbukwa wawili hao kwa maana ya Harmonize na Paula walikuwa hawaelewana baada ya habari kuvuja mwaka jana kwamba Harmonize alikuwa anamvizia hali ya kuwa alikuwa pia katika mahusiano na mamake, Kajala.

Sakata hilo lilizua chuki katika makundi mawili, Harmonize akakosana na Kajala na pia msanii mwenzake Rayvanny ambaye ndiye alikuwa katika mahusiano na binti huyo kipindi hicho.

Mwaka huu baada ya Harmonize kujitutumua kwa kila namna kuweka mambo wazi baina yake na Kajala, walirudiana na kuvishana pete za harusi, jambo ambalo huenda ndilo pia limepiga pasi hata tofauti kati ya bintiye na Harmonize.

Msanii Harmonize sasa amekuwa akimmiminia sifa kocho bintiye wa kupanga Paula kwenye mitandao huku akisema kwamba anamuonea Fahari kama Tajiri mdogo baada ya kufungua duka lake la kuuza nguo.

“Yaani nakuonea Fahari sana @therealpaulahkajala, Tajiri mdogo Oyaaa. Nani anaweza kufanya Bora kuliko Binti yangu,” Harmonize aliandika kwenye video yenye huyo binti alifanya na kuipakia kwenye Instagram.