Hadi umeanza kufanana na Karen Nyamu - Shabiki amwambia Samidoh

Shabiki huyo pia alimkumbusha Samidoh kuwa Nyamu ni mkewe wa pili

Muhtasari

• Wengi walisema kwamba dhana ya watu wawili kufanana baada ya kukaa pamoja kimapenzi kwa muda ni kweli.

Samidoh aambiwa anafanana na Nyamu
Samidoh aambiwa anafanana na Nyamu
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Mugithi ambaye pia ni afisa wa polisi Smauel Muchoki almaarufu Samidoh alipakia klipu kwenye ukurasa wake wa TikTok akisikiliza ngoma za Mugithi. Mashabiki wake wamemiminika hapo kumsifia kutokana na utanashati wake.

Katika klipu hiyo, Samidoh anaonekana akiwa nadhifu shati jeupe na tabasamu zimemtoka ghaya.

Kilichogeuka kuwa gumzo katika mtandao huo ni maoni ya shabiki mmoja ambaye alisema kwamba kwa kweli Samidoh wamefanana na mzazi mwenziwe, seneta maalum Karen Nyamu.

Kulingana na shabiki huyo, dhana kuwa watu wakiishi pamoja kwa muda mrefu huwa wanafanana hatimaye ni kweli kwani aliona msanii Samidoh panda lake la uso ukilitathmini kwa muda la lile la seneta Nyamu basi moja kwa moja unapata majibu sawa.

Shabiki huo hataq hivyo hakusitia kumwambia Samidhoh maneno hayo na hata kumkumbusha kwamba Nyamu ni mke wake wa pili.

“Haki hadi umeanza kufanana na Karen Nyamu, mkeo wa pili,” Shabiki kwa jina Mag Wanjiku alimkumbusha Samidoh.

Baadhi ya mashabiki wake walizungumzia maoni haya ya Wanjiku wengine wakiyapuuzilia mbali na wengine wakikubaliana kwamba ni kweli Samidoh alikuwa anaonekana kama Nyamu baada ya kuzaa watoto wawili naye.

“Nilifikiri nilikuwa naona mambo yangu hapa,” mwingine aliandika.

Itaumbukwa hivi majuzi Samidoh alionekana kwenye majengo ya bunge la seneti ambako Nyamu alikuwa anakula kiapo kuhudumu kama seneta maalum na picha zao zilipasua mitandao ya kijamii kwa madai kwamba huenda wamerudiana tena.