(+screengrab) Karen Nyamu amshauri Samidoh jinsi ya kukaa na wanawake 2 bila tatizo

Nyamu alipakia meme ya kuonesha jinsi mwanaume anaweza ishi na wanawake wawili pasi na kutokea matatizo ya kawaida.

Muhtasari

• “Wakati una wake wawili na hutaki wazidi kugombana au kuwa na matatizo yoyote,” meme hiyo imeandikwa.

Karen Nyamu ampa Samidoh ushauri jinsi ya kuishi na wake wawili
Karen Nyamu ampa Samidoh ushauri jinsi ya kuishi na wake wawili
Image: instagram

Katika siku za hivi karibuni, afisa wa polisi na ambaye pia ni msanii wa Mugithi Samwel Muchoki almaarufu Samidoh amejipata katika ugomvi wa wake zake mitandaoni.

Karen Nyamu na Edday Nderitu ni wanawake ambao wote wamemzalia Samidoh na inaaminika msanii huyo anawakubali na kuwapenda wote, licha ya Edday kuonekana kutofurahia suala la mke mwingine katika ndoa yake.

Picha lilianza wakati msanii Samidoh alijitokeza wazi na kukiri kwamba yeye na Nyamu ni wapenzi na katika penzi lao la siri walikuwa wameshazaa mtoto pamoja, alimuomba msamaha mke wake wa kwanza Edday ni kuahidi kutomsaliti tena.

Lakini baada ya miezi michache, Samidoh na Nyamu tena walionekana pamoja na miezi kadhaa baadae seneta huyo maalumu akaonekana ni mjamzito ambao alisema ni wa msanii Samidho.

Hili liliyumbisha uhusiano wake na mke wake wa kwanza mpaka fununu kuibuka kwamba ndoa yao ilisambaratika.

nyamu karen
nyamu karen

Edday amekuwa akionekana kulaumu wanawake walupo kwa kile anasema wanafaa kuheshimu ndoa za wanawake wengine kwa kukoma kutoka kimapenzi wa wanaume ambao wameoa.

Sasa msanii Samidoh amebaki katikati ya Sakata hilo asijue pa kuenda kati ya Edday na Nyamu, ambaye juzi walionekana naye katika majengo ya bunge wakati wa kuapishwa kwa maseneta.

Karen Nyamu kupitia Instagram story yake alipakia picha moja ambayo ni meme ikionekana kumlenga Samidoh kwa ushauri. Nyamu alipakia picha hiyo ikionesha mwanaume aliyewapamba wake zake wawili kwa nguo mfanano na kusema hilo ndio suluhishi kwa mtu mwenye hataki ugomvi kati ya wake zake.

Picha hiyo inaonesha mwanaume amevalia nguo yenye rangi zake zimegawanyika mara mbili kati kati na kila mwanamke amesimama upande ambapo rangi ya nguo zake inafanana na upande wa nguo za mwanaume.

“Wakati una wake wawili na hutaki wazidi kugombana au kuwa na matatizo yoyote,” meme hiyo imeandikwa.