Karen Nyamu hatimaye afichua jina la mtoto wake wa pili na Samidoh

Muhtasari

•Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh anaaminika kuwa baba wa mtoto huyo wa tatu wa Karen.

Mwanasiasa Karen Nyamu
Mwanasiasa Karen Nyamu
Image: RADIO JAMBO

Hatimaye mwanasiasa na wakili mwenye utata mwingi Karen Nyamu amefichua jina la mtoto wake wa tatu.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Karen alipakia video fupi akimkumbatia binti huyo wake mchanga na kufichua kuwa jina lake ni Wairimu.

Haijulikani ikiwa mtoto huyo mwenye umri wa mwezi mmoja unusu atatumia jina la babake kuwa jina lake la tatu ama atachukua la mamake.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh anaaminika kuwa baba wa mtoto huyo wa tatu wa Karen.

Wawili hao ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya siri kwa muda mrefu wana mtoto mwingine mmoja wa kiume, Sam Juniour ambaye alizaliwa mwaka wa 2020.

Wairimu alizaliwa mnamo Februari 26, mwaka huu.