Vera Sidika atoa msaada kwa mama aliyetaka Ksh 200 ya chakula

Mwanadada huyo alisema ndio alikuwa amezaa na kukosa hela za chakula ambapo alikuwa anataka msaada.

Muhtasari

• Mwanadada baada ya kupokea hela zile alitaka kulia ila Sidika akamwambia asilie ni kawaida mtu kuhitaji msaada.

Vera sidika asema hawezi chumbiana na watu wa reggae
Vera sidika asema hawezi chumbiana na watu wa reggae
Image: instagram

Mwanasosholaiti Vera Sidika ametia joto mioyo ya mashabiki wake wengi baada ya kudokeza kuwa alimsaidia mama mmoja aliyekuwa amezaa na kukosa chakula kwa ajili ya kujitia nguvu.

Sidika alipakia kwenye instastory yake, mwanasosholaiti huyo alipakia mazungumzo baina yake na mwanadada huyo aliyeonekana kufika mwisho wa reli kabisa na alikuwa anataka japo kitu kidogo kama shilingi mia mbili tu kwa ajili ya chakula.

Sidika wala hakusita na kumuuliza maswali mengi bali aliguswa moja kwa moja na hali yake na kumtaka mwanadada huyo kutuma namba yake ya miamala ya M-Pesa kwa ajili ya kumsaidia.

Mwanadada huyo alipompa namba yake Sidika alimrushia hela kwenye MPesa na mwanadada akajawa na furaha ghaya huku akimsifia Sidika kwa kumsaidia na kumshukuru kwani alikuwa ameona kiza kabisa mbele nyuma.

Sidika alisema kwamab haijalishi unapitia nini katika maisha haya bali kuonesha mtu furaha kidogo kadri ya uwezo wako ni jambo zuri sana ambalo utafanya kujiletea thawabu maishani mwako.

“Ukarimu kidogo kwa watu unaenda mbali sana na kuwa mkubwa. Wacha sisi wote tujali wenzetu wenye matatizo,” Vera Sidika aliandika kwenye picha hiyo.

Mwanadada huyo alimwambia Sidika kuwa hakuwa anategemea ukarimu huo kutoka kwake na alijawa na machozi ya furaha ambapo Sidika alimwambia asilie kwani ni hali ya kawaida tu kusaidia.