Cartoon Comedian atafuta mtaalamu wa mapenzi

Cartoon alitaka kujua jinsi watu huweza kuondoka katika uhusiano na kuwa wenye furaha baada ya kuachana

Muhtasari

• Hii ni baada ya Cartoon kufichua kwamba mpenzi wake ambaye bado hajatambulika mtandaoni alimsaliti kimapenzi na kupiga jaramba na mrembo mwingine.

Image: Cartoon Comedian Instagram

Mcheshi wa kike nchini Kenya na mwanamuziki aliyeanza kuimba hivi majuzi Cartoon Comedian afichua kuwa anatafuta mtaalamu wa mapenzi kwa kuwa maisha yamekuwa magumu mno.

Cartoon alitaka kujua jinsi watu huweza kuondoka katika uhusiano na kuwa wenye furaha baada ya kuachana na mpenzi wao kwa sababu ameshindwa kuwa mwenye kuhimili uchungu wa kukatika kwa uhusiano wake.

"Niko karibu kurukwa na akili, mtaalamu yoyote wa mapenzi tafadhali nitafute,"alisema.

Image: Caroon Comedian instagram

Rafiki yake alisema kuwa hapendi kumwona Cartoon katika hali ambayo yumo saa hii alimpa moyo na tumaini mcheshi huyo na kumhakikishia kuwa mambo yatakuja kuwa shwari.

Alimuunga Cartoon kuuliza swali alilokuwa akiuliza.

"Sasa mbona alicheat,"aliuliza rafiki yake Cartoon.

Hii ni baada ya Cartoon kufichua kwamba mpenzi wake ambaye bado hajatambulika mtandaoni alimsaliti kimapenzi na kupiga jaramba na mrembo mwingine.

Cartoon alisema kuwa hisia zake ziliumizwa na kuwa hayuko sawa kiasi cha kutaka kujitenga na mitandao ya kijamii ili hisia zake zituliye kwanza.

“Nimekuwa nikiumia kidogo, baada ya kuvunjika kwa mahusiano yangu. Nilifikiria mimi nitakaa mgumu kama Taliban lakini nimegundua mimi ni mtoto wa kike mdaifu. Nitarudi baada ya kujikusanya na kupona. Mbona unacheat?” Cartoon Comedian aliuliza kwa hisia za uchungu.

Cartoon alieleza hisia zake kwa kuweka ishara ya moyo uliovunjika kuonyesha kuwa hisia zake zimevunjwa na kuumizwa kimapenzi.