Mwanaume anatakiwa awe vizuri kitandani na pia awe na pesa - Justina Syokau

Nina pesa Mungu amenibariki, naweza weka mwanaume lakini sitaki - Justina Syokau

Muhtasari

• Hapa Nairobi tumekuja kufanay kazi. Ni uchague kufanya kazi au urudi nyumbani - Syokau.

Syokau awakemea vijana wanaomtaka bila kuwa na pesa
Syokau awakemea vijana wanaomtaka bila kuwa na pesa
Image: Instagram

Mwanamuziki Justina Syokau ameibua mjadala mitandaoni kwa nyingine tena akisema kwamba yeye amebarikiwa ako na pesa nyingi ila hawezi kumweka ndani mwanaume.

“Nina pesa Mungu amenibariki, naweza weka mwanaume lakini sitaki,” Justina alijigamba kwa mikogo ya tausi.

Akizungumza katika mahojiano na blogu moja ya mitandaoni, Justina alisema kwamba hata kwenye DM yake wanaume wengi wamejaa wakimwambia kwamba wako vizuri upande wa pili kitandani lakini upande wa mfuko ndio kidogo wana kiangazi.

Alisema kwamba sababu yake ya kutowataka wanaume wenye uwezo wa aina yake kitandani licha ya kuwa wakavu mifukoni ni kuwa jijini Nairobi watu wameenda pale kwa ajili ya kufanya kazi na kutafuta pesa, na kama mwanaume hawezi kujisimamia kifedha basi heri arudi alikozaliwa.

“Hapa Nairobi tumekuja kufanay kazi. Ni uchague kufanya kazi au urudi nyumbani. Mimi nataka mwanaume mchapa kazi anayechakarika, mtu amabye anaweza leta kitu mezani. Vijana wanasema ati ooh sina pesa lakini niko sawa kitandani, kwani mimi ndio wa bure? Mwanaume anatakiwa awe vizuri kitandani na pia ajiongeze kifedha,” Justina alisema.

Kando na hayo, mwanamuziki huyo ambaye haijulikani kama anaimba nyimbo za injili ama za kidunia aliweka wazi kuwa yeye yuko tayari kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mafuta katika utumbo wa chini almaarufu Liposuction ili kuboresha mwili wake amabo alisema ni kwa utukufu wa Mungu tu wala si kuwafurahisha watu kwa mshepu wa kutisha.