Huddah: Siku moja nitaandika kitabu, nitamwaga udaku wote wa mahusiano ya kibiashara

Alitupilia mbali uwezekano wa kutoa mswada huo kwa njia ya video kwa kile alisema anachukia video sana.

Muhtasari

• Mfanyibiashara huyo alisema kuwa atasimulia kwa undani mahusiano ya kibiashara na mashabiki wake itabidi wamejiweka tayari.

Image: Huddah

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amedokeza kwamba hivi karibuni atajiunga na kwenye orodha ya watu maarufu mitandaoni kutoka nchini Kenya ambao waliwahi kuandika vitabu.

Kupitia Instastories zake, mfanyibiashara huyo wa vipodozi alisema kwamba siku moja ataandika kitabu kitakachonuia kuwapa mawaidha ya kibiashara watu ambao wana mawazo ya kuwekeza katika biashara.

Alisema kwamba kitabu hicho kitakuwa na mawaidha chungu nzima kuhusu jinsi ya kufanikiwa kibiashara na aliwahakikishia mashabiki wake kuwa watapenda kile ambacho atawaelezea.

Akionekana kusisitiza msimamo wake kwa njia ya video, Huddah alisema kwamba yeye tangu siku za nyuma hajawahi kuvutiwa kufanya mambo yake kwa njia ya video bali kwa simulizi za maandishi.

Mwanashosholaiti Huddah atangaza kuandika kitabu chake
Mwanashosholaiti Huddah atangaza kuandika kitabu chake
Image: Instagram

“Siku moja nitaandika kitabu changu cha biashara. Sio cha kupendeza kama inavyoweza kuonekana. Mtajua kuwa nachukia video. Kwa hivyo maarifa yote utalazimika kupata kutoka kwa kitabu. Sababu nitamwaga udaku mwingi kuhusu biashara na mahusiano ya kibiashara. Itabidi nyote mmekubaliana,” Huddah Monroe alidokeza.

Hivi karibuni, Huddah amekuwa akionekana kutokuwa sawa kiakili na mpaka wakati mmoja kudokeza kuwa hayuko katika hali yake ya kawaida. Vile vile ameonekana akitunga jumbe za kumrejelea Mungu.

“Mungu Mpendwa, hivi majuzi nimekuwa nikihisi kutokuwa imara na baadhi ya sehemu zangu kutaka tamaa. Mimina neema zako na rehema zako juu yangu,” Huddah aliandika.

Iwapo atafanikiwa kuandika kitabu hicho basi atakuwa kwenye rodha ya wanawake maarufu waliowahi kuandika vitabu vya kusimulia maisha yao akiwemo Lilian Ng'ang'a na Akothee.