Sio dhambi kumchukia mtu, mimi namchukia Alikiba - Baraka the Prince

Kila mtu ana adui, na mimi adui wangu ni Alikiba - Baraka the Prince.

Muhtasari

• "Ni kweli halafu mimi siwezi kumficha mtu. Kwa hiyo kumchukia mtu sio dhambi na haikatazwi kumchukia mtu,” Baraka the Prince alisisitiza.

Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Baraka the Prince, Alikiba Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Image: Instagram

Wiki kadhaa zilizopita msanii Baraka the Prince alivunja mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba hampendi aliyekuwa rafiki wake wa muda mrefu, msanii     Alikiba.

Aliyasema haya katika moja ya tamasha mkoani Mwanza, kaskazini mwa Tanzania akiwa jukwaani ambapo mashabiki wake walimtaka kutumbuiza wimbo wake alioshirikiana na Alikiba enzi akiwa katika lebo ya Kings Music.

Kwa mshangao mkubwa, mashabiki walipata jibu la ukaidi kutoka kwake akikataa katakata kutumbuiza wimbo huo kwa kile alisema kwamba hataki kabisa kulisikia jina la Alikiba karibu naye kwani linamchefua.

Wengi wlaihisi msanii huyo hakuwa katika hali yake razini kiakili na kumtuhumu kuwa huenda alikuwa ametumia vilevi vya kumfanya kuzungumza vile ila tena aliposhuka kutoka jukwaani aliradidi maneno yale yale kwamab hampendi Alikiba, katika mahojiano na wanablogu.

Juzi pia amesisitiza msimamo wake huo katika mahojiano na kituo kimoja cha habari ambapo amesema hampendi Alikiba ila akagoma kabisa kuzungumzia kilichozua ufa baina yao au kile kinachowagombanisha.

“Ni kweli halafu mimi siwezi kumficha mtu. Kuna vitu vinaitwa vya kibinafsi ambavyo mimi siwezi kuvizungumzia. Ukiishi ukisema kwamba unaezakuwa unawapenda watu wote huo ni unafiki. Kila mtu ana maadui. Kwa hiyo kumchukia mtu sio dhambi na haikatazwi kumchukia mtu,” Baraka the Prince alisisitiza.

Alijitetea kwa kusema kwamba hata mtoto mdogo anapozaliwa tu tayari ana maadui ambao wanamuona na kumchukia wakati yeye hana tatizo wala laana yoyote. Alisema kwamba Alikiba atasalia kuwa adui wake mkubwa ila akabaki kwenye njia yake kuu kutofichua kiini cha uadui wake na mfalme huyo wa Bongo Fleva.