Eric Omondi apongezwa kwa kumuonesha Churchill heshima, miaka 14 tangu kumleta runingani

Churchill wikendi iliyopita alikuwa anasherehekea miaka 45 ya kuzaliwa na Omondi alimsifia pakubwa.

Muhtasari

• “Napenda jinsi ambavyo unamtambua Mwalim Churchill muda wote. Mungu akubariki,” shabiki mmoja kwa jina Mercy Anyango alimwambia.

Wacheshi Eric Omondi na Churchill
Wacheshi Eric Omondi na Churchill
Image: Maktaba

Mchekeshaji Eric Omondi amemsherehekea Mwalimu Churchill akifikisha umri wa miaka 45.

Kupitia ukurasa wake wa Instahram, Omondi alipakia klip kadhaa za video ambazo zinaonesha jinsi Churchill alimkuza na kumlea katika Sanaa ya uchekeshaji na kumshukuru kwa kumshika mkono kwa muda huo wote kuanzia zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Churchill ni mcheshi kuu nchini Kenya ambaye kupitia kipindi chake cha Churchill kwenye runinga pamoja pia na kuwa na matamasha kadhaa kote nchini, ameweza kuwalea wachekeshaji wengi amab owanatambulika leo hii.

Omondi alimmiminia sifa na kusema kwamab kamwe hatokaa kumsahau Churchill kwa wema aliomuonesha na kumtambulisha kwenye Sanaa ya ucheshi ambayo ni ngumu sana kuwafanya watu wacheke na uchumi huu ulivyoporomoka kuliko bei ya mitumba.

Churchill alikuwa anasherehekea miaka 45 wikendi iliyopita ambapo mchekeshaji Omondi alikuwa bado yupo nchini Uganda kwa hafla ya ucheshi na ndio maama Jumatatu asubuhi aliamkia na kumwandikia ujumbe huo japo kwa kuchelewa lakini aliutambua mchango wake mkubwa kwenye Sanaa ya ucheshi Kenya.

“Siku zote nitakuwa mwenye fadhila kwako baba, siku njema ya kuzaliwa hata kama kwa kuchelewa Mwalimu. Mungu akupe Maisha Marefu, Miaka Zaidi na Baraka zaidi. @mwalimchurchill,” Omondi aliandika.

Hii si mara ya kwanza kwa mcheshi huyo kumtambua bayana Churchill kwa mchango mkubwa kwani katika tamasha mbalimbali huwa anamtaja kama mmoja wa wat uwaliomuokota na kumpa nafasi ya kuchekesha katika runinga.

Mashabiki wake walimhongera kwa hilo na kusema kwamba ndio maana anazidi kukwea ngazi za mafanikio kwenye tasnia ya ucheshi kwa zaidi ya miaka 15.

“Napenda jinsi ambavyo unamtambua Mwalim Churchill muda wote. Mungu akubariki,” shabiki mmoja kwa jina Mercy Anyango alimwambia.

“Unajua kwanini nakuheshimu @ericomondi ni kwa sababu hii 👆.....Bado unamheshimu mwalimu Churchill mpaka sasa...nakuvulia kofia mkubwa,” mwingine kwa jina Simply Momanyi alimwambia.