Vera Sidika kusherehekea miaka 10 ya umaarufu, kutajwa sana kwenye ngoma za wasanii

Sidika alisema tafrija hiyo itafanyika Jumamosi Desemba ya tarehe 17.

Muhtasari

• "Nimekuwa maarufu kwa miaka 10 na mnamo Desemba 17, nitasherehekea miaka 10 ya kuwa maarufu,” Sidika alisema.

Vera Sidika
Vera Sidika
Image: Instagram

Vera Sidika, mwanafasheni ambaye pia ni mwanasosholaiti mstaafu amejipiga kifua kuwa wiki kesho atasherehekea kudumu kwa miaka 10 kama mwanasosholaiti na mtu maarufu ambaye amekuwa akitajwa sana kwenye nyimbo za wasanii wa ndani na nje ya Kenya.

Sidika alikuwa akijibu swali la shabiki wake mmoja aliyetaka kujua jinsi anavyojihisi anapotajwa kweney ngoma za wasanii na kila mtu kumzungumzia mitandaoni.

“Huwa unajihisi aje wakati wasanii haswa kutoka Tanzania wanapokutaja kwenye mashairi yao ya ngoma,” shabiki alitaka kujua.

“Kusema kweli mimi ndiye mtu maarufu kutoka Kenya ambaye ametajwa sana kwenye ngoma za wasanii. Nimekuwa maarufu kwa miaka 10 na mnamo Desemba 17, nitasherehekea miaka 10 ya kuwa maarufu,” Sidika alisema.

Alisema tarehe hiyo pia itakuwa kumbukumbu ya kusherehekea ndoa ya wazazi wake huku akisema ni kama ujauzito wake ulitungwa Desemba ya mwaka 88 na umaarufu wake ukaanza tarehe kama hiyo lakini mwaka tofauti.

“Hii pia itakuwa kumbukumbu ya harusi ya wazazi wangu, ni kama ujauzito wangu ulipatikana Desemba 17 mwaka 1988, nikazaliwa miezi 9 baadae na umaarufu ukaja tu tarehe na mwezi sawia, mwaka tofauti,” Sidika alitamba.

Mama huyo wa mtoto mmoja pia alifutilia mbali uvumi kuwa yuko mjamzito tena na kusema kwamba yeye anamshughulikia bintiye Asia Brown kuanza shule mwaka kesho Januari.

Asia Brown miezi michache iliyopita alikuwa anasherehekewa na wazazi wake Vera Sidika na Brown Mauzo kufikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa.