Vera Sidika avunja kimya kuhusu madai kuwa ni mjamzito

Vera Sidika ameonekana akificha tumbo lake, jambo lililowafanya wanamitandao kudai ni mjamzito

Muhtasari

• Kwenye Instagram, Sidika alikana madai hayo na kusema kuwa ni tumbo la baada ya kujifungua na kuwa ameongeza kilo.

• Sidika alisema picha zinazoenea ni za mwaka jana.

Vera Sidika na Brown Mauzo
Image: Vera Sidika Instagram

Mwanasosholaiti Vera Sidika amevunja kimya kuhusu madai kuwa ni mja mzito kwa mara ya pili.

Wanamitandao wamekuwa wakidai kuwa mama huyo ni mjamzito kwani amekuwa akificha tumbo lake akienda mahali popote.

Kwenye Instagram, Sidika alikana madai hayo na kusema kuwa ni tumbo la baada ya kujifungua na kuwa ameongeza kilo.

" Mbona muamini hayo? Hii ilikuwa mwaka jana nilipokuwa na mimba ya Asia na nilificha nikiwa nimevalia nguo hii. Aki watu wanaweza kueneza uvumi," Sidika alisema kupitia kipindi cha maswali na majibu Instagram.

Alipakia video hiyo akionyesha mimba ili kuwakumbusha wanamitandao kuwa ilikuwa mwaka jana.

Hata hivyo, wanamitandao wamekuwa na uhakika kuwa mwanasosholaiti huyo ni mjamzito.

Katika kipindi hicho, Sidika pia alifichua kuwa amepanga kumpeleka mtoto wake Asia Brown shuleni mwaka ujao 2023, Januari.

Alieleza jinsi bintiye amekuwa mkubwa, hata kuanza kukimbia na mwenye hamu ya kutaka kujua mengi.

"Asia ataenda shule Januari na nina imani kuwa atafurahi sana kwani anapenda watoto. Yeye huchangamka anapoona watoto wenzake, nafurahia hilo. Hata kama wanachopenda kufanya ni kucheza siku nzima, hilo ni jambo nzuri kwake," mpenzi huyo wa Brown Mauzo alisema.

Hivi majuzi, katika jibu lake, mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 33 alifichua kwamba yeye na mumewe wanapaga kufunga pingu za maisha  kanisani mwishoni mwa mwaka ujao ama mwanzoni mwa mwaka wa 2024.

"Mimi ni mtu anayependa ukamilifu kwa hivyo ningetaka kuchukua wakati kupanga kila kitu kwa ukamilifu," alisema.

Mara kadhaa katika siku za nyuma Vera aliwahi kuweka wazi kuwa yupo kwenye ndoa halali na mwimbaji huyo kutoka Pwani.