Ahsante Mungu, sasa nimeokoka! - Esma Platnumz baada ya vipimo vya HIV

Esma amekuwa kwa mahusiano kadhaa ambayo hayajazaa matunda mema kwa upande wake.

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto wawili miaka miwili iliyopita aliondoka kwenye ndoa yake akisema mumewe aikuwa na jicho la nje.

Esma aokoka baada ya kupata majibu ya HIV
Esma aokoka baada ya kupata majibu ya HIV
Image: Instagram

Mjasiriamali Esma Platnumz ambaye pia ni dadake mkubwa msanii nguli Diamond Platnumz ameonesha furaha yake baada ya kuchukua vipimo vya janga la UKIMWI na majibu kutoka kuwa yu mzima.

Kupitia instastory yake, Esma Platnumz alipakia majibu hayo na kwa furaha akasujudu na kutoa shukrani kwa Mungu huku akiahidi kuwa sasa kwenda mbele ataokoka kabisa na hatoingia katika mahusiano ambayo yatahatarisha hali yake ya afya.

“Ahsante Mungu, sasa ndugu zangu nimeokoka rasmi,” Esma aliandika.

Esma ni mmoja kati ya wanadada wa kisasa wenye tija na ufanisi mkubwa maishani lakini nyota ya ndoa imewakataa kabisa, au tuseme imekawia kuwaangazia.

Itakumbukwa mwanadada huyo muuza madera na mitandio ya wanawake bado yuko singo zaidi ya miaka miwili tangu kuachana na mfanyibiashara mashuhuri kwa jina Msizwa waliyepatana nchini Afrika Kusini.

Msizwa alimuoa Esma kama mke wake wa tatu katika sherehe ya harusi iliyotangazwa sanamwezi Julai 2020 kati kati ya janga la Korona, lakini waliachana miezi mitatu baada ya harusi yao.

Mapema mwezi wa Novemba 2020, mama huyo wa watoto wawili alifichua kwamba aliachana na ndoa hiyo kwa sababu mwanamume wake alikuwa na jicho la nje. Wake wa kwanza na wa pili wa Msizwa wanaishi Afrika Kusini na watoto wao, na mara nyingi yeye husafiri kwa ndege kutoka Tanzania kwenda kuwa na familia zake mbili.

Hadi muungano wake na Msizwa, Esma alikuwa bado katika uhusiano usio na mwelekeo dhabiti na babake mtoto Petit Man Wakuache. Petit ameoa na wanashirikiana na dadake Diamond kulea mtoto wao.