Mke wangu alisafiri, kwa mara ya kwanza nimerudia boxer - Terence Creative

Mchekeshaji huyo alisema kuwa amejua umuhimu wa mke baada ya mkewe kusafiri kidogo.

Muhtasari

• Wengine walimkandia kwa kumuuliza kuwa kwani umuhimu wa mkewe ni katika kuosha nguo za ndani.

Terence Creative akimla denda kali mpenzi wake Milly Chebby.
Terence Creative akimla denda kali mpenzi wake Milly Chebby.
Image: Instagram

Mchekeshaji na mwigizaji Terence Creative amezua utani kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa kwa mara ya kwanza tangu waoane na  mkewe Milly Chebby, amelazimika kurudia nguo ya ndani.

Terence alisema kuwa mkewe alisafiri na ndio maana alilazimika kurudia nguo ya ndani kwani ana uvivu sana kufua.

Mchekeshaji huyo alizua utani kuwa ndio mara ya kwanza anajua umuhimu wa mke katika ndoa kwani muda wote ndiye amekuwa akifanya kazi ya kumfulia nguo zote lakini safari hii kwa kuwa yuko mbali, hangeweza kufanya udhubutu wa kujifulia bali akaona jawabu la haraka ni kurudia tu.

Niko singo kwa muda 😂😂😂😂 tangu mpenzi wangu @millychebby asafiri, ndio nimejua umuhimu wa bibi. Kwa mara ya kwanza nimerudia boxer,” Terence Creative aliandika Instagram.

Msanii huyo wa vichekesho alipakia picha akiwa anamla denda la kishua mkewe huku akimuaga na mabegi mazito ya kibabe.

Mashabiki wake ambao wanadadisi maisha ya familia hiyo walimtania na kutaka kujua kama ana mwanandani moja tu huku wakisema kuwa mkewe hajaondoka siku nyingi zilizopita kwenda safarini.

“Si ni Jana tu ametoka kwani uko na moja,” Chesir Jnr alimuuliza.

“Sasa kama unakumbuka boxer ndio umerudia mara moja, soksi utakumbuka kweli ni lini ulivaa mara ya mwisho?” mwingine alimuuliza.

“Nyie mnajua wakati mwingine ni kuchelewa sana na pia wanaume wengi huchukulia kawaida kuwa na mke safi pia,” Ero Collections alimwambia.

Wanadada wengine walisimulia jinsi wapenzi wao wa kiume waliwapigia simu kuwauliza jinsi ya kufanya badhi ya mambo wakati walisafiri mbali nao kwa siku chache.

“Kama hujapiga simu kuelezewa jinsi ya kuwasha gesi uko sawa, nguo utavumilia,” mmoja alimwambia kwa utani.