Hivi ni kwa nini Lavalava amesahaulika kimuziki? Msanii mwenzake ajibu, chanzo hiki hapa

Msanii Dulla Makabila alitaja suala la uchawi kutumwa WCB Wasafi ili kuizima nyota ya Lavalava kiasi kwamba amesahaulika kimuziki.

Muhtasari

• Lavalava ni mmoja kati ya wasanii wa mwanzo kabisa waliosainishwa mkataba katika lebo ya Diamond.

• Lakini wasanii wa nyuma kama Mbosso na Zuchu wamefanikiwa pakubwa kumshinda katika lebo hiyo ya Wasafi.

Msanii Lavalava
lavalava, Msanii Lavalava
Image: Instagram

Kwa muda mrefu kumekuwa na uzushi na minong’ono kutoka kwa baadhi ya watumizi wa mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa msanii Lavalava kutoka Wasafi kwenye gemu la muziki.

Msanii huyo ambaye amekuwa katika lebo ya WCB Wasafi kwa muda mrefu kila uchao anatoa ngoma lakini wengi wamekuwa wahisi kuwa nyimbo zake hazisikiki kabisa kama zilivyokuwa zikisikika kkatika miaka yake ya mwanzoni akiwa Wasafi.

Baada ya kuondoka kwa Harmonize na Rayvanny, Wasafi ilibaki na kiongozi wake Diamond Platnumz na wasanii wengine watatu wakiwemo huyo Lava lava, Mbosso na Zuchu.

Lakini cha ajabu ni kwamba miziki ya Diamond, Mbosso na Zuchu ndio pekee inaendelea kutamba na kuteka anga huku Lavalava nyimbo zake zikiwa hazisikiki hata kidogo licha ya kujikita katika utunzi na uandishi wa mashairi mazuri kila uchao.

Ssa baadhi wanahisi kuwa huenda msanii huyo amepigwa kipapai kwa maana ya kufanyiwa uchawi kiasi kwamba nyimbo zake hata aimbe vipi bado hazitusui kwenye mitandao ya kijamii wala kwenye vyombo vya habari.

Mmoja wa wale wenye dhana hiyo ni msanii wa nyimbo za singeli kutoka nchini Tanzania, Dulla Makabila ambaye katika wimbo wake wa hivi karibuni ambao unazidi kutamba kwa jina ‘Pita Huku’ ameibua madai hayo kuwa wachawi ndio wamepeleka uchawi Wasafi hata Lavalava akiimba hasikiki kabisa.

“Mchawi ndio chanzo cha umasikini, unapitia kwenye vipembe hivi milango huioni. Na uchawi mkaupeleka usafini, yaani Lavalava hata aimbe vipi haonekani…” vesi hiyo ya mwisho kabisa kwenye wimbo huo inasema.

Hivi, wewe unahisi ni kwa nini Lalalava hasikiki kwa sana siku hizi kama awali? Je, kuna ukweli gani kwa huu wimbo wa Makabila kuhusu uchawi, unakubaliana na kauli hiyo?