Nilikuwa milionea nilipokuwa miaka 17-KRG the Don ajigamba

Krg alisema kuwa anaunda urithi utakaomfanya akumbukwe na Wakenya kwa miaka 650 ijayo.

Muhtasari
  • Alisema kwa sasa yeye ni tajiri kuliko wasanii wote wa Kenya kwa pamoja
  • Alisema kuwa itamchukua mwanamuziki wote wa Kenya, miaka 10 ya kufanya kazi kwa bidii ili kuwa tajiri katika kiwango chake cha utajiri
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: KRG the Don

Mmoja wa wanamuziki tajiri maarufu wa dancehall nchini Kenya, Krg the Don amesema kwamba alikuwa milionea alipokuwa na miaka 17 kwa sababu alikuwa na busara sana, na aliwekeza vizuri sana pesa ndogo alizopata.

Akizungumza katika mahojiano na Mungai Eve, Krg ameendelea kusisitiza kuwa yeye ndiye msanii tajiri zaidi nchini Kenya.

Krg alisema kuwa anaunda urithi utakaomfanya akumbukwe na Wakenya kwa miaka 650 ijayo.

Alisema kwa sasa yeye ni tajiri kuliko wasanii wote wa Kenya kwa pamoja.

Alisema kuwa itamchukua mwanamuziki wote wa Kenya, miaka 10 ya kufanya kazi kwa bidii ili kuwa tajiri katika kiwango chake cha utajiri.

Kulingana na Krg, pesa ndio kila kitu na huwa anafikiria jinsi atakavyoongeza faida yake na ndio maana huwa anatembea na matajiri.

Krg alisema kuwa anatoza Ksh.1 Milioni kwa kutumbuiza katika onyesho lolote la Arena.

Kwa uchezaji wa vilabu anatoza ksh.500000 , kwa kila uchezaji na hiyo ndiyo sababu yeye hucheza mara chache katika vilabu, kwa sababu vilabu vingi haviwezi kumudu.

Aliendelea na kusema kwamba anatoza ksh.250,000 , kwa kufuata watu kwenye Instagram.

Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwa sababu, yeye ni brand na pia ni mshauri kwa wengi.

Krg alisema kuwa yeye hategemei muziki, anafanya kwa burudani tu. Alisema kuwa yeye ni mfanyabiashara aliyefanikiwa sana na ni miongoni mwa mabilionea watano bora nchini Kenya.