Amber Lulu afichua jinsi amekuwa akipokea kichapo cha mbwa kutoka kwa mpenziwe

Mwanamuziki huyo amedai kuwa mwanamume huyo hata ameapa kumuua na kuongeza kuwa anaogopa kwenda nyumbani.

Muhtasari
  • Amber aliongeza kuwa anachukia jinsi mwili wake unavyoonekana mbaya kutokana na majeraha aliyopata
Amber-Lulu-eating-food(1)
Amber-Lulu-eating-food(1)

Aliyekuwa mpenzi wa Prezzo raia wa Tanzania Amber Lulu ameweka paruanja madai ya kudhulumiwa na mpenzi wake kwa kumpiga.

Mwanamuziki huyo  amedai kuwa mwanamume huyo hata ameapa kumuua na kuongeza kuwa anaogopa kwenda nyumbani.

Kwa mujibu wa Lulu, anapigwa kwa kumfanyia kazi mtoto wake.

"Daa nimekuwa mtu wa kuhangaika na kuteseka pasiposababu ya msingi mapenzi niliyo nayo kwa mtoto wangu na uchungu na uvumilivu Mungu pekee ndio anajua kuna muda najitoa kufanya chochote kwa ajili ya mwanangu

Nilizaa kwa mapenzi na mapenzi ya Mungu ila nachofanyiwa kama sina haki kuna muda natamani kumkumbatia mwanangu nishinde nae nashindwa coz nisipo hangaika mwanangu atakula nn??Nyumba nalipa na nn??

Leo napigwa kama mbwa,kisa kumwangaikia mwanangu naumia sa ivi mtu ananitishia kuniua Mungu," Lulu alifichua kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Amber aliongeza kuwa anachukia jinsi mwili wake unavyoonekana vibaya kutokana na mapigo aliyopata.

"Mpaka naogopa kurudi nyumbani kwangu mtoto wangu namuita hotel kuangalia mwili wangu kama daaah."

Siku za nyuma, Lulu alidai kuwa babake mtoto alikuwa akimnyanyasa hata alipokuwa mjamzito na kuongeza kuwa hana budi kuvumilia.

"Katika mahusiano, mambo haya ni ya kawaida sana lakini kama wanawake, tunapaswa kuvumilia. Siwezi kuzungumza mengi kuhusu hilo kwani linaweza kumuathiri mume wangu na mtoto wangu na familia jambo ambalo si zuri."