"Wewe unanitosha" - Wema Sepetu amwambia Whozu, akidokeza kumzalia

Wema amekuwa akikashifiwa kwa kutoka kimapenzi na Whozu ambaye ni mdogo kiumri kumliko.

Muhtasari

• Wema alidokeza kuwa amebakisha kitu kimoja kumfanyia Whozu ili kukamilisha maisha yake, ila hakukitqaja kitu hicho.

Image: Instagram

Mwigizaji mkongwe Wema Sepetu anazidi kummwagia mpenzi wake Whozu makopakopa ya mapenzi kwa mtindo wa aina yake akiahidi kuwa yeye tu amemtosha katika maisha yake.

Mwigizaji huyo ambaye wiki jana alijipata katika sakata la kuishi kwa nyumba ya msaada na mpenzi wake Whozu, alijitapa kuwa anajihisi mwenye bahati kuwa katika uhusiano na msanii huyo.

Wema alidokeza kuwa amebakisha kitu kimoja kumfanyia Whozu ili kukamilisha maisha yake, ila hakukitqaja kitu hicho.

Baadhi walihisi alikuwa anamaanisha kumzalia mtoto na wengine wakilonga kuwa huenda alikuwa anapanga kufunga ndoa naye na kutulia kabisa.

Mebakisha kimoja tu kukamilisha furaha yangu kwako Amore... Tuseme Inshallah...🤲🏼🤲🏼🤲🏼 Lakini pia hata isipokuwa, yote ninayoyajua ni kwamba wewe unanitosha ... nakupenda siku zote mpenzi wangu,” Wema Sepetu aliandika.

Wema alipakia rundo la picha wakiwa wamevaa mavazi mfanano na Whozu wakijivinjari.

Mwigizaji huyo tangu aweke uhusiano wake wazi na Whozu mwaka jana, amekuwa akipokea maneno ya hila za kila aina kutoka kwa nyomi ya watu ambao wamekuwa wakimsuta kutoka kimapenzi na Whozu, ambaye ni mdogo kiumri kumliko.

Hata hivyo, licha ya safari hii kudai kuwa Whozu anamtosha, mwaka jana alipakia video kwenye App yake akisema kuwa haoni kama uhusiano wake na msanii huyo utafika hatua ya kuvishana pete na pengine kufanya ndoa.

Waigizaji wengine ambao wamejipata katika mkondo huo wa kutoka kimapenzi na wanaume wagodo kiumri ni pamoja na Kajala aliyechumbiana na Harmonize, Aunty Ezekiel anayechumbiana na msanii Kusah, miongoni mwa wengine.