Hatimaye Rayvanny atoa tamko lake baada ya Ex wake Paula Kajala kufanya harusi

Paula alidokeza jana kufunga harusi ya Kiislamu na mwanamume aliyemtambulisha kama Ally.

Muhtasari

• “Hongera sana P.. na iwe heri,” Rayvanny aliandika kwenye picha hiyo.

• Mama yake pia alimhongera na kumtaka kuwa mke bora na si bora mke.

Alichokisema Rayvanny baada ya Paula kuolewa
Alichokisema Rayvanny baada ya Paula kuolewa
Image: Facebook

Msanii Rayvanny ameoneka ukomavu wa akili baada ya kumtakia aliyekuwa mpenzi wake Paula Kajala kheri njema baada ya binti huyo kudokeza kwamba ameolewa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Rayvanny alipakia picha ya Paula akiwa anavishwa pete na mwanamume kwa jina Ally na kumhongera kwa hatua hiyo ambayo ni ndoto kwa kila mwanamke.

“Hongera sana P.. na iwe heri,” Rayvanny aliandika kwenye picha hiyo, na kupokelewa kwa maoni mseto kutoka kwa maelfu ya mashabiki wake mtandaoni.

Hata hivyo, ndoa ya Paula imezua vijembe mitandaoni, idadi kubwa ya watu wakionekana kutoamini kama kweli ni ndoa au ni kiki tu anafukuzia suala la harusi.

Mrembo huyo ambaye ni mtoto wa pekee wa Kajala, kutoka familia ya Kikristo alipakia picha akiwa anavishwa pete ka kutokana na picha hizo, ni Dhahiri kwamba ni ndoa ya Kiislamu. Hata hivyo, hakuonesha uso wala sura ya mwanamume huyo Ally – jambo ambalo lilizidisha kutoamini kutoka kwa wengi wa wanamitandao.

Kando na Rayvanny, mama yake Kajala Masanja pia alimhongera binti yake kwa kufanikiwa kuitia ndoa mfukoni na kumpa usia wa mama,

“Mungu akutangulie katika maisha yako haya dada Pau, ukawe mke bora na si bora mke,” Kajala alimwandikia.

Kinachowafanya wengi kutoamini kwamba kweli Paula ameolewa ni hatua ya kupakia picha pasi na kuonesha sura ya huyo mume wake mpya, na pia hatua ya kutumia mstari wa kionjo cha wimbo wa Rayvanny kumtambulisha mpenzi huyo mpya – “mwamba huyu hapa”

Kuolewa kwake kunakuja miezi michache baada ya mama yake Kajala kutengana na aliyekuwa mchumba wake Harmonize, licha ya wawili hao kuvishana pete katika sherehe maalum iliyozungumziwa kwa miezi kadhaa mnamo mwezi Juni mwaka 2021.