Jimal: Mimi sijawahi omba radhi kwa Amira nikitaka turudiane, ni yeye aliniandikia!

Jimal pia alisema aligundua Amira alikuwa anakunywa pombe na kuvuta sheesha kwa nyumba yake.

Muhtasari

• Amira alimwandikia ujumbe wa msamaha na kumtaka Jimal kuupakia kwenye ukurasa wake Instagram, Jimal alisema.

Jimal asema hakuwahi omba msamaha kwa Amira
Jimal asema hakuwahi omba msamaha kwa Amira
Image: Instagram, Screengrab

Zogo baina ya waliokuwa wanandoa Jimal Rohosafi na Amira linazidi kuchukua mkondo changamano baada ya mfanyibiashara huyo kukanusha kwamba hajawahi muomba Amira radhi akitaka warudiane.

Jimal katika mahojiano alisema kwamba msamaha uliionekana kwenye ukurasa wake wa Instagram mwaka jana haukuwa wake bali ni mke wake Amira alichukua simu yake na kuandika kabla ya kuupakia.

Alisema kwamba Amira alikuwa anamtaka kuomba msamaha njia sawa na ile ya Harmonize alikuwa akimuomba Kajala msamaha kwa kumnunulia zawadi za gari na mikufu ya dhahabu ili kuonesha kwamba kweli amejutia kumsaliti kimapenzi na Amber Ray.

“Siku moja tumeketi akaniambia kwamba kama nilitaka kumuomba msamaha basi nifanye hivyo kwa sauti na kishindo. Nikamwambia acha nikuambia pole ujue imetoka kwa roho yangu, akaniambia hapana na kutaka nifanye hivyo kwa mitandao ya kijamii. Basi nikampa simu akaandika vizuuri ujumbe ule na kunitumia na kuniambia andika hiyo, hadi picha akanitumia ya kuweka. Akachukua simu yangu na kupakia msamaha ule katika ukurasa wangu,” Jimal alisema.

Jimal alisema kwamba alipigwa na butwaa baada ya kuona Amira akienda Tanzania na kusema kwamba angerudi ili kutangazia mashabiki wake taarifa muhimu na kwamba hakumsamehe.

Kwa hasira, alimzomea Amira kwamba Amber Ray alimfanya kuwa maarufu mitandaoni baada ya zogo lililowahusisha wote watatu. Kwa wakati mmoja alimtaka kumheshimu Amber ambaye katika mahojiano hayo, alionekana kumtetea sana mwanasosholaiti huyo.

“Nilijaribu kumbembeleza hapa na pale, nikajaribu kumweka vizuri, wazazi na marafiki wakamuongelesha lakini mambo hayakuenda vizuri kwa sababu nahisi mpaka sasa hivi ni ustaa umemuingia kwa kichwa chake,” Jimal alisema.