Harmonize kubadili dini kuwa Mkristo? Christina Shusho afichua walichozungumza

Miezi mitatu iliyopita, wasanii hao wawili walipatana kwa ghafla nchini Kenya na Harmonize alimkimbilia na kumbusu Shusho miguuni.

Muhtasari

• Shusho alisema kwamba moja ya kitu alifurahi kusikia kutoka kwa msanii huyo ni kumtamkia kuwa alipenda kuisikiliza miziki yake ya injili.

Shusho na Harmonize wafanya mazungumzo ya kubadili dini
Shusho na Harmonize wafanya mazungumzo ya kubadili dini
Image: Instagram

Christina Shusho, msanii wa muda mrefu wa injili kwa mara ya kwanza amefunguka walichozungumza na Harmonize mwaka jana walipokutana ghafla nchini Kenya, na Harmonize akamkimbilia na kumbusu miguuni.

Katika mahojiano maalum na kituo kimoja cha habari nchini Tanzania, Shusho alisema kwamab baada ya kitendo kile kilichonaswa na mapaparazzo, walikwenda chemba faraghani na kuwa na mazungumzo kwa upana.

Shusho alisema kwamba moja ya kitu alifurahi kusikia kutoka kwa msanii huyo ni kumtamkia kuwa alipenda kuisikiliza miziki yake ya injili.

“Nilipata nafasi ya kukaa naye kuzungumza, aliongea kitu ambacho kiligusa moyo wangu sana, akasema dada mimi napenda sana nyimbo zako, unapoimba nyimbo zako, unatuelimisha kuhusu Mungu, unatuelekeza kumjua mungu na hutulazimishi, unatuachia sisi chaguo la kuamua tumfuate Mungu au tuendelee na mambo yetu...” Shusho alinukuu maneno ya kutoka moyoni mwa Harmonize.

 Alisema kwamba msanii huyo pia alimalizia kwa kumtamkia kwa sauti ya hakika kwamab kutokana na himizo analolipata kutoka kwa nyimbo zake, siku moja atamuona kanisani.

“Hicho kinanifanya mimi nasiiliza sana nyimbo zako, navutiwa sana kutaka kujua hicho unachokiimba. Na nina uhakika siku moja, utaniona kanisani,” Shusho alinukuu maneno ya Harmonize.

Inafahamika vizuri tu kwamba Harmonize ni Muislam na Shusho ni Mkristo ambaye mwaka jana alianzisha kanisa lake na tamko la kwamba Harmonize siku moja atatimba kanisani na Shusho ni ishara kwamba anawaza kubadili dini kutoka Uislam hadi Ukristo.

Shusho alisema kwamba tamko hilo la Harmonize lilimpa himizo kubwa akajua kwamba kumbe kuna watu mbali mbali anaowagusa na kuwaweka karibu na Mungu kupitia uimbaji wake.