Mrembo ajitokeza na kudai ni mtoto wa Pelé, adai kupata mgao wa urithi wake

Mrembo huyo anadai kwamba Pele aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mama yake miaka ya 1980s kupelekea kuzaliwa kwake.

Muhtasari

• Mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia alikuwa amelazwa hospitalini mjini Sao Paulo tangu mwishoni mwa Novemba kabla ya kifo chake Desemba 29.

• Mchezaji huyo, ambaye alifariki kutokana na saratani ya utumbo mpana akiwa na umri wa miaka 82 mnamo Desemba 29 mwaka jana, alikuwa na watoto saba rasmi.

Marehemu Pele wa Brazil.
Marehemu Pele wa Brazil.
Image: Mail

Mwanamke anayedai kuwa mtoto wa siri wa gwiji wa soka Pele anajaribu kupata kipande cha mali ya marehemu mwanasoka huyo.

Mchezaji huyo, ambaye alifariki kutokana na saratani ya utumbo mpana akiwa na umri wa miaka 82 mnamo Desemba 29 mwaka jana, alikuwa na watoto saba rasmi.

Sasa, mrembo Maria do Socorro Azevedo anadai mamake aliwahi kuchuana na mshindi wa Kombe la Dunia katika miaka ya 1980. Atakuwa na kipimo cha DNA ili kubaini kama Pele analingana naye vinasaba.

Mwishoni mwa mwaka jana punde baada ya kifo chake, inadaiwa kwamba Pele aliacha wosia ambao aliorodhesha mtoto huyo wa kambo japo jina lake halikuwekwa wazi.

Chanzo kimoja kiliiambia The Mirror: ‘'Pele alitaja katika wosia wake kuwepo kwa Maria do Socorro Azevedo, ambaye anaweza kuwa binti yake, na akaeleza rasmi kwamba lazima apokee sehemu ya mali yake ikiwa kipimo cha DNA kitathibitisha baba yake.”

Binti wa kambo wa Pele Gemima Lemos McMahon pia anawasilisha ombi kwa mahakama za Brazil kutajwa mrithi wa Pele. Mama yake, Assiria alikuwa mke wa pili wa Pele.

Mali yake inaaminika kuwa na thamani ya kati ya Pauni Milioni 12 na Pauni Milioni 75.

Mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia alikuwa amelazwa hospitalini mjini Sao Paulo tangu mwishoni mwa Novemba kabla ya kifo chake Desemba 29.

Pele aliibuka kidedea akiwa na umri wa miaka 17 kwenye Kombe la Dunia la 1958, na kuisaidia Brazil kupata rekodi ya kwanza kati ya rekodi zao tano za mafanikio katika shindano hilo.