Kila taifa ulimwenguni kuita uwanja kwa jina la Pelé - Rais wa FIFA, Gianni Infantino

Infantino alisema FIFA itatuma ombi hilo kwa kila taifa kote ulimwenguni ili Pele apate kuenziwa ifaavyo.

Muhtasari

• Pele anatarajiwa kuzikwa Jumanne katika makaburi ya ghorofa nchini Brazili.

• Inaarifiwa kuwa alichagua kuzikwa katika ghorofa ya 9 ya makaburi hayo yenye ghorofa 14.

FIFA yataka kila nchi kuita uwanja mmoja kwa jina la Pele
FIFA yataka kila nchi kuita uwanja mmoja kwa jina la Pele
Image: PA Images

Rais wa FIFA Gianni Infantino ametangaza mipango ya shirikisho hilo la soka duniani kuomba mataifa yote, kila moja kuita angalau uwanja mmoja kwa jina la aliyekuwa muasisi wa soka Brazil, Pele kama njia moja ya kumpa heshima.

Pele alifariki mwishoni mwa mwaka jana katika hospitali moja nchini Brazil akiwa na miaka 82 baada ya kupambana na ugonjwa kwa muda mrefu.

Infantino, ambaye yuko Brazili kwa mazishi ya Pele, aliwaambia waandishi wa habari, "Tutaomba kila nchi ulimwenguni kutaja mojawapo ya viwanja vyao vya soka kwa jina la Pele."

Mnamo Aprili 2021 Rio de Janeiro iliachana na mpango wa kuupa uwanja maarufu wa Maracanã baada ya Pelé baada ya kupingwa na gavana wa jimbo hilo.

Jeneza la Pele liliwekwa ndani ya uwanja wa Vila Belmiro huko Santos Jumatatu, uwanja wa nyumbani wa kilabu ambapo alitumia takriban maisha yake yote.

Pele anatarajiwa kuzikwa leo hii Jumanne katika makaburi ya ghorofani katika kile ambacho majarida yaliripoti kuwa alichagua kuzikwa katika ghorofa ya 9 ya makaburi hayo ili kuendelea kutazama kwenda uwanja wa timu ya Santos ambayo aliitumikia kwa muda mrefu na kupata umaarufu kupitia timu hiyo.

Inaarifiwa kuwa mkongwe huyo wa soka alichagua kuzikwa katika ghorofa ya 9 mnamo mwaka 2003 na uamuzi wake huo ni kutokana na namba 9 ya jezi ambayo baba yake mzazi alikuwa anavalia enzi akiwa mchezaji pia, kwa maana hiyo alichagua kuzikwa katika ghorofa ya tisa kama njia moja ya kumuenzi baba yake.

Ghorofa hilo la makaburi lina ghorofa 14.