Utahitajika kumlipa mwanasosholaiti Shakilla Ksh 6,600 ili kujibu meseji yako kwenye DM

Shakilla alitangaza bei hii mpya muda mchache baada ya akaunti yake ya Instagram kuwa 'verified'

Muhtasari

• Shakilla amekuwa akizungumziwa kwa njia tofauti, haswa baada ya mwaka jana kudai kwamba hakika hayuko sawa kutokana na kuburuzwa vikali mitandaoni.

Shakilla ashangaa wanaume kumkwepa
Shakilla ashangaa wanaume kumkwepa
Image: Instagram

Mwanasosholaiti wa Kenya mwenye utata mwingi, Shakilla ametoa bei mpya ya wale watakaotaka kujibiwa jumbe zao kwenye faragha yake ya Instagram – DM.

Shakilla alitangaza hili saa chache tu baada ya ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi Zaidi ya laki tatu na nusu kudhibitishwa na mamlaka ya Meta inayomiliki Instagram.

“Hakika nimepewa tiki ya samawati na Instagram, hatimaye. Sasa DM zenu zitakuwa zinajibiwa kwa bei ya dola 50 (sawa na shilingi 6600 za Kenya). Ahsante sana,” Shakilla aliandika.

Hivi majuzi, kulikuwa na tetesi mitandaoni kwamba msanii huyo ambaye hayuko nchini alienda nchi za Uarabuni kujivinjari baadhi wakisema kwamba alikwenda kuigiza filamu zenye maudhui ya watu wazima.

Shakilla amekuwa akizungumziwa kwa njia tofauti, haswa baada ya mwaka jana kudai kwamba hakika hayuko sawa kutokana na kuburuzwa vikali mitandaoni.

Baada ya kubainisha kwamba alikuwa na uchu wa kuigiza filamu za watu wazima, baadae mwanasosholaiti huyo aliibuka tena miezi michache iliyopita akionesha wasiwasi wake kuwa hakuna mwanamume aliyetaka kuchumbiana na yeye, akihisi kwamba pengine alizaliwa kuwa mtu wa mitaani tu na wala si mke wa ndoa.

“Kwa hiyo tuseme katika wanaume wote ambao wananifuata Instagram hakuna hata mmoja anayetaka kuingia katika uhusiano wa hakika na mimi. Kwani mimi nilikusudiwa kuwa wa mitaani katika maisha yangu yote bila familia?” Mwanasosholaiti huyo aliuliza kwa wasiwasi mkubwa.

Umaarufu wa mwanasosholaiti huyo ulikua kwa kasi mwaka 2020 wakati wa janga la Covid-19 alipotambulishwa na Xtian Dela kwenye kipindi kilichonuia kuwawezesha wasanii kutumia muda wao vizuri wakati huo ambao shughuli nyingi zilisimama.