• Wiki mbili zilizopita, Psquare walijinunuliwa majumba ya kifahari London na Atlanta mtawalia.
Mwimbaji wa Nigeria Joseph Akinwale almaarufu Joeboy amejinunulia nyumba mpya
Mwimbaji huyo, ambaye alifahamisha hayo kwa wafuasi wake alipokuwa akionesha picha za nyumba yake mpya aliyoinunua kwenye akaunti yake ya Instagram siku ya Jumapili, aliandika, “LAVIDA BOY”
Mwanamuziki mwenzake, Mr Eazi, alimpongeza na kuthibitisha kuwa nyumba hiyo ni ya nne ya ununuzi wake wa mali isiyohamishika akisema, “Crib Number 4!!! Ni nzuri hii!!!!!!!”
Hata hivyo, haikubainika Zaidi mijengo mitatu ya kwanza msanii huyo aliinunua linin a wapi, sambamba na mjengo huu wa hadhi ya nyota tano ambao maelezo yake kuhusu sehemu ulipo na uligharimu kiasi kipi cha pesa, ni finyu sana.
Wiki chache zilizopita, wasanii kutoka kundi la P-Square, mapacha Peter na Paul Okoye pia walidokeza kusafiri kwenda Marekani ili kujipatia mali.
Wasanii hao kila mmoja alijitapa kwenye akaunti ya Instagram kwamba wamefanikiwa kujinunulia nyumba.
Rudeboy ambaye jina halisi ni Paul Okoye alionyesha nyumba yake ya Atlanta ambayo tayari alikuwa ameinunua akishiriki picha na video za ndani ya jumba hilo la kifahari.
"Nyingine #ATL," aliandika
Ndugu yake Peter naye alisema kuwa alikuwa mjini London Uingereza kujinyakulia jumba lake, akisema kuwa uchaguzi wa Nigeria uliokumbwa na misukosuko mingi iliyokaribia kutishia usalama na Amani ya taifa hilo uliwafunza mengi – wakiashiria kwamba hatua yao ya kujinunulia nyumba nje ya Nigeria ni njia moja ya kujihakikishia usalama endapo hali itadhoofika nchini mwao kutokana na mawimbi ya kisiasa.