Tiffah, Binti wa Diamond ataka mjakazi kufutwa kazi kwa kufoka jina lake

Alimtaka mama yake kuchukua hatua la sivyo afikishe suala hilo kwa babake nchini Tanzania.

Muhtasari

• Akionesha jinsi mjakazi huyo alifoka jina lake, Tiffah alisema kuwa kitendo hicho hakikumfurahisha na kutaka mamake kuchukua hatua ya kumpiga kalamu.

Tiffah amtaka mjakazi wao kufutwa kazi kwa kufoka jina lake.
Tiffah amtaka mjakazi wao kufutwa kazi kwa kufoka jina lake.
Image: Instagram

Binti kifungua mimba wa Diamond Platnumz na mwanamitindo Zari Hassan, Tiffah ametaka mjakazi wa nyumbani kwao nchini Afrika Kusini kufutwa kazi mara moja kisa kufoka jina lake wakati alikuwa anamwita.

Katika video fupi ambayo ilipakiwa kwenye ukurasa wa binti huyo wa Instagram, alikuwa anazungumza na mama yake, Zari alikuwa anamuuliza ni nini kilimchukiza na binti wa watu kwa madaha ya mwana wa mfalme akadamka kuwa tabia ya mjakazi wao wa ndani haikumfurahisha.

Alimtaka mama yake kuchukua hatua la sivyo afikishe suala hilo kwa babake nchini Tanzania.

“Nah hakuna anayetakiwa kuniita hivyo....naipokeza na menejimenti. Meneja wa tawi katika SA au sivyo nitaipandisha ofisi kuu Tanzania,” Binti huyo alisema.

Zari alimuuliza binti yake pendekezo angetaka lichukuliwe, binti Tiffah alidamka kwa kusisitiza kwamba angependa mjakazi huyo kufutwa kazi.

“Afutwe kazi!” Tiffah alisema.

Hata hivyo, mamake alimtaka kuchukua uamuzi toafauti wa kujaribu kumfikia mjakazi huyo na kumuongelesha jinsi angependa awe akimwiita badala la kumfokea.

Lakini mtoto huyo alisisitiza kwamba uamuzi wake wa kutaka mjakazi kufutwa ndio wa mwisho na angetaka utekelezwe na mamake la sivyo atafikisha malalamishi kwa babake Diamond, Tanzania.