Rayvanny amwaga machozi ya furaha akiwashukuru Wakenya kufanya wimbo wake namba moja

Bosi huyo wa lebo ya Next Level alisema kuwa upendo wa Wakenya siku zote humpa sababu ya kutamani kuwa Mkenya vile vle.

Muhtasari

• Video hiyo ya Rayvanny ambaye alimshirikisha mama mtoto wake kama Vixen ilitoka wikendi iliyopita na kupata mapokezi makubwa.

•Mpaka sasa, wimbo huo una watazamaji zaidi ya milioni moja kwenye jukwaa la YouTube chini ya siku tatu.

Rayvanny na Fahyvanny wakioneshana mahaba mazito baharini kwenye boti.
Rayvanny na Fahyvanny wakioneshana mahaba mazito baharini kwenye boti.
Image: Screengrab//Instagram

Msanii wa Bongo,Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny amefichua kuwa wakati mwingine anajihisi kama Mkenya.

Hili linajiri baada ya mashabiki w wake wa Kenya kumfanya nambari moja katika wimbo wake na aliyekuwa mpenzi wake Fayvanny kwenye mtandao wa You Tube hivyo kumfanya msanii huyo kueleza furaha yake kwa uungwaji mkono ambao Wakenya wanampa.

Rayvanny vile vile aliwashukuru mashabiki wake wa Tanzania kwa kuwa pia alikuwa anaongoza kwenye majukwa na chati ya Daily chats huku akionyesha kuwa anawaenzi watanzania pia kwa upendo wao kwake

"Aki kuna muda huwa najiona Mkenya kabisa,,Forever nafasi ya 1 Kenya.... nambari 1 Tanzania kwenye Daily Charts," alisema Rayvanny.

Video ya Wimbo wake wa Forever imefikisha watazamaji milioni 1.2 ndani ya siku mbili.

Rayvanny hivi majuzi walirudiana na aliyekuwa mpenzi wake Fahyvanny baada ya kutengana kwa miaka mitatu.

Hili lilidhihirika walipotoa kibao cha Forever pamoja naye huku akiahidi kumpenda Fahyvanny daima kwenye wimbo huo.

Rayvanny alimmiminia sifa mpenzi wake kwa  urembo wake asilia na kusema kuwa atakuwa kando yake kila wakati.

Rayvanny na Fahyvanny waliwachana mwaka wa 2020 kisha Vanny akachumbiana na mwana wa Fridah Kajala, Paula Kajala.

Hata hivo, walipata matatizo katika mahusiano yao baada ya madai kuwa Harmonize alimmezea mate Paula ilhali alikuwa kwenye mahusiano na mamake ambaye ni Frida.

Fahyma alimshutumu Rayvanny kwa kutojali familia .

Mashabiki wa Rayvanny walifurahia wimbo wao na kuchumbiana kwa Rayvanny na Fahyma kwa mara nyingine