Baada ya Rayvanny kurudi kwa Fahyvanny, Marioo achukua nafasi yake moyoni mwa Paula Kajala

Paula alianza kudokeza mapenzi na Marioo wiki moja baada ya Rayvanny kudokeza kurudiana na mama mtoto wake, Fahyvanny.

Muhtasari

• Mwijaku hata hivyo alimshauri Marioo kuwa makini na Paula akisema kuwa mwanadada huyo aliwahi waambukiza Harmonize na Rayvanny ugonjwa wa UTI.

Marioo na Paula waoneshana mapenzi mubashara.
Marioo na Paula waoneshana mapenzi mubashara.
Image: Insatgram

Msanii Marioo na binti wa mwigizaji mkongwe Fridah Masaja, Paula Kajala wanazidi kuoneshana mapenzi mitandaoni.

Wawili hao ambao wanatajwa kuwa ni kiki wanafukuzia au pengine ni wimbo mpya ambao Marioo anatarajiwa kutoa video yake na kumtumia Paula kama Vixen, wamekuwa wakisifiana kwa maneno ya kimahaba kwa wiki moja sasa.

Jumatano Paula alipakia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram na Marioo akawa mtu wa kwanza kufika pale na kummwagia makopakopa kuwa ndiye moyo wake.

Pia Paula hakukawia kujibu akimtaja kuwa mtu wake pendwa Zaidi.

“Moyo wangu,” Marioo aliandika akiongeza na emoji ya mapenzi.

“Binadamu wangu pendwa,” Paula alimjibu pia akimalizia na emoji hiyo hiyo ya mapenzi.

Hili liliwaacha watumizi wa Instagram wakizungumza kuhusu uwezekano wao kuwa kwenye uhusiano ambao ndio mwanzo unachipukia.

Wiki moja baada ya kuanza kutumiana jumbe za mapenzi, mtangazaji mbwatukaji Mwijaku alimwandikia Marioo ujumbe akimtaadharisha kutoshiriki mapenzi na Paula peku, kwa kile alidai kuwa mwanadada huyo hapo nyuma ana historia ya kuwaambukiza Harmonize na Rayvanny na ugonjwa wa zinaa.

Paula alianza kuonekana wazi akitangaza nia yake ya kuwa kwenye mapenzi wiki mbili tu baada ya aliyekuwa mpenzi wake Rayvanny kudokeza kurudiana na mama wa mtoto wake Fahyvanny, ambapo pia alimshirikisha kwenye video ya wimbo wake wa ‘Forever’.

Rayvanny alikuwa kwenye mapenzi na Paula kuanzia mwaka 2021 lakini mwaka 2022 waliacha kuonekana pamoja mitandaoni, kila mmoja akizifuta picha walizopiga pamoja na hivyo wadadisi wa mitandaoni kuhisi kuwa mambo hayakuwa sawa katika himaya na Vanny Boy.

Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza wazi kukiri kuhusu kuachana.