Paula Kajala ajibu baada ya kudaiwa kuwaambukiza Harmonize na Rayvanny UTI

Mwijaku alimuomba Marioo kutumia mipira akidai Paula aliwaambukiza mastaa hao magonjwa ya zinaa .

Muhtasari

•Mwijaku alimuonya Marioo kumhusu Paula akidai kwamba aliwahi kuwaambukiza Harmonize na Rayvanny magonjwa ya njia ya mkojo. 

•Paula, kwa kejeli alimkosoa Mwijaku kwa kuiita dawa hiyo ya kutibu bakteria mwilini 'power safe' badala ya 'Powercef'.

Harmonize, Paula, Ravanny
Image: HISANI

Mwanamitindo Paula Paul Kajala hatimaye amevunja kimya baada ya muigizaji Burton Mwemba almaarufu Mwijaku kuibua madai kwamba aliwaambukiza Harmonize na Rayvanny magonjwa ya zinaa katika siku za nyuma.

Wiki iliyiopita, Mwijaku alimuonya Marioo kumhusu binti huyo wa muigizaji Frida Kajala Masanja huku akidai kwamba aliwahi kuwaambukiza mastaa hao wawili wa bongo magonjwa ya njia ya mkojo. 

Muigizaji huyo alidai wawili hao walilazimika kudungwa sindano kadhaa  ili kuponywa na hivyo kumsihi Marioo kujikinga.

"Utumie mpira mdogo wangu maana Mmakonde na Vanny Boy walitibu U.T.I na sindano tano powersafe. @marioo_tz," alisema.

Hii ilikuwa baada ya mwimbaji huyo kudokeza mahusiano na Paula.

Huku akijibu madai ya mtangazaji huyo wa Clouds Media, mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20, kwa kejeli alimkosoa Mwijaku kwa kuiita dawa hiyo ya kutibu bakteria mwilini 'power safe' badala ya 'Powercef'.

"Ni powercef sio power safe jamani," aliandika kwenye Instagram.

Katika siku kadhaa za hivi majuzi, Paula ameonekana akijivinjari na staa wa Bongo, Omary Mwanga almaarufu Marioo na kumekuwa na vidokezo kuwa atashirikishwa kwenye video ya wimbo ijayo wa mwanamuziki huyo.

Haijabainika ikiwa wawili hao wanatoka kimapenzi lakini kwa hakika wamekiri kupendana. Siku ya Jumamosi, Marioo alisifu urembo wa mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 na kubainisha kuwa anampenda.

"Imagine mtoto mbichi kama huyu alafu anakupenda.. @therealpaulahkajala #ananipenda inakuja hivi karibuni," Marioo aliandika chini ya video ya Tiktok ya Paula akicheza wimbo wake mpya 'Ananipenda.' 

Huku akijibu kwenye chapisho hilo la Instagram, binti huyo wa muigizaji Kajala Masanja alisema laiti wangekutana awali.

"Natamani ningekutana nawe awali," aliandika na kuambatanisha na emoji zilizoashiria mahaba mazito kwake.

Marioo aliendelea kumtambua mwanamitindo huyo kama kipenzi chake.

Matukio haya yalijiri takriban wiki moja tu baada ya Rayvanny na Fahyma almaarufu Fayvanny  kuthibisha kufufuka kwa mahusiano yao yaliyosambaratika takriban miaka mitatu iliyopita. Hii ni baada ya bosi huyo wa Next Level Music kumshirikisha mzazi huyo mwenzake katika video ya wimbo wake mpya 'Forever.'

Rayvanny na Paula wanaaminika kuchumbiana 2021 kabla ya kutengana katika hali tatanishi. Harmonize alidaiwa kujaribu bahati yake kwa mwanamitindo huyo wakati akichumbiana na mama yake, Kajala Masanja.